Nchi ya Guinea imeruhusiwa kuandaa michuano ya Kimataifa ya soka, kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miezi 17.
Hatua hii imekuja baada ya Shirika la afya duniani WHO kuitangaza nchi hiyo kuwa huru dhidi ya maambukizi ya Ebola.
Hakikisho hilo limetolewa na Shirikisho la soka barani Afrika CAF, kupitia Katibu Mkuu Hicham El Amrani, kwa rais wa Shirikisho la soka nchini Guinea.
Hii inaamanisha kuwa Guinea watacheza mchuano wake nyumbani jijini Conakry dhidi ya Malawi mwezi wa tatu katika mchuano wa kufuzu kucheza fainali Afrika mwaka ujao nchini Gabon.
Guinea iko katika kundi moja na Malawi, Zimbabwe na Swaziland na wamekiuwawakichezea mechi zao nchini Morroco mjini Casablanca.
Kundi L
Mechi Ushindi Alama
Swaziland 2 1 4
Zimbabwe 2 1 4
Malawi 2 0 1
Guinea 2 0 1