Connect with us

Chipolopolo (Zambia)

CHAN 2016: Rwanda na DRC kuchuana robo fainali

CHAN 2016: Rwanda na DRC kuchuana robo fainali

Rwanda itamenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika robo fainali ya michuano ya soka barani Afrika kuwania taji la CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani.

Michuano hii inaendelea kwa wiki ya pili katika viwanja mbalimbali nchini Rwanda.

Rwanda ilifuzu baada ya kumaliza ya kwanza katika kundi la A kwa alma 6, mbele ya Ivory Coast ambayo pia ilifuzu ikiwa pia na alama 6 lakini kwa uchache wa mabao ikilinganishwa na Rwanda.

Rwanda-CHAN-2016

Mchuano wa DRC na Rwanda, utapigwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali na ni mchuano ambao unatarajiwa kuzua hisia kubwa baina ya mashabiki wa nchi zote mbili.

Uwanja wa Amahoro unatarajiwa kufurika kwa maelfu ya mashabiki na licha ya Rwanda kuwa nyumbani mashabiki wa DRC wanatarajiwa kuvuka mpaka kuishangilia Leopard.

Mashabiki wa timu zote mbili walitamani sana mataifa hayo jirani yangekutana katika fainali ya taji hilo na kombe hilo kubaki katika eneo la Afrika ya Kati, lakini hili halijatimia.

Mara ya mwisho kwa mataifa haya yote kukutana ilikuwa ni mapema mwezi huu katika mchezo wa kirafiki kabla ya kuanza kwa michuano hii na Rwanda waliifunga DRC bao 1 kwa 0.

Lomalisa Mutambala of DR Congo celebrates during the 2016 CHAN Rwanda, match between DR Congo and Angola at the Huye Stadium in Butare, Rwanda on 21 January 2016 ©Muzi Ntombela/BackpagePix

Cameroon nayo itakabiliana na Ivory Coast katika robo fainali nyingine pia siku ya Jumamosi katika uwanja wa Huye mjini Butare.

Timu ya Cameroon ilifuzu baada ya kumaliza ya kwanza katika kundi B kwa 7 mbele ya DRC, huku Ivory Coast ikimaliza ya pili katika kundi A kwa alama 6.

Mara ya mwisho kwa timu hizi mbili kukutana, ilikuwa ni mwaka 2015 katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika, mchuano ambao Ivory Coast waliishinda Cameroon bao 1 kwa 0.

Siku ya Jumanne, michuano ya kunatamatisha kundi la C inachezwa katika uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali na Umuganda mjini Gisenyi kuanzia saa 10 jioni saa za Afrika ya Kati.

1453751320Cameroon's-Yazid-Atouba-vies-for-the-ball-against-DR-Congo's-Franck-Mfuki-during-the-final-Group-A-match-at-Huye-stadium

Niger itachuana na Tunisia huku Guinea ikimenyana na Nigeria.

Timu zote nne zina nafasi ya kufuzu katika hatua ya robo fainali ikiwa zitapata ushindi leo.

Nigeria inaongoza kundi hilo kwa alama 4, ikifuatwa na Guinea na Tunisia ambazo zote zina alama 2 huku Niger ikiwa na alama 1.

Isaac Chansa of Zambia fouls Farai Madhananga of Zimbabwe during the 2016 CHAN football match between Zimbabwe and Zambia at the Rubavu Stadium in Rubavu, Rwanda on 19 January 2016 ©Gavin Barker/BackpagePix

Siku ya Jumanne, mechi za kundi D pia zitatamatishwa. Zambia ambayo imeshafuzu katika hatua ta robo fainali itamaliza mchuano wake wa makundi dhidi ya Mali ambayo ni ya pili kwa alama nne, huku Uganda wakimenyana na Zimbabwe ambayo imeshaondolewa katika mashindano haya.

Krahire Yannick Zakri of Ivory Coast celebrates with teammates during the 2016 CHAN Rwanda, match between Morocco and Ivory Coast at the Amahoro Stadium in Kigali, Rwanda on 20 January 2016 ©Muzi Ntombela/BackpagePix

Mechi za nusu fainali zitachezwa tarehe 3 na 4 mwezi Februari huku fainali ikichezwa tarehe 7 katika uwanja wa Amahoro.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in Chipolopolo (Zambia)