-
by
Victor Abuso
Sunday Oliseh amejiuzulu kuwa kocha wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria, Super Eagles.
Hatua hii inakuja miezi saba baada ya kupewa kibarua hicho na Shirikisho la soka nchini humo NFF.
Mchezaji huyo wa zamani wa Super Eagles alitangaza kujiuzulu kwake, kupitia ukurasa wake wa Twitter kwa kile alichokisema NFF imevunja masharti ya mkataba wake.
Aidha, anadai kuwa Shirikisho la soka nchini humo limeshindwa kumuunga mkono katika kazi yake, kutomlipa marupurupu yake pamoja na wachezaji wake.
“Kwa sababu ya kutoheshimiwa kwa mkataba wangu, kutoungwa mkono, kutolipwa marupurupu yangu pamoja na yale ya wachezaji wangu, najiuzulu kama kocha wa Super Eagles,” aliandika Oliseh kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Pamoja na hayo, Oliseh amewashukuru raia wa Nigeria kwa kumuunga mkono wakati alipokuwa kocha wa timu ya taifa.
Mwaka uliopita, Oliseh alitofautiana na kipa Vincent Enyeama, na baadaye akaamua kustaafu kuichezea timu ya taifa.
Shirikisho la soka nchini Nigeria linasema bado halijapokea rasmi barua ya Oliseh kuonesha kujiuzulu kwake.
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
CAF Champions League
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns Off to a Lukewarm Start in 2024/25 CAF Champions League
CAF Champions League
AL Ahly start CAF CL campaign with win over Stade d’Abidjan
CAF Confederation Cup
Simba make good start beating Bravos do Maquis
CAF Confederation Cup
Enyimba fall to Al Masry in Alexandria
CAF Confederation Cup
Zamalek got their Group D campaign off to a comfortable star
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...