Connect with us

Lweza FC waiangusha Vipers FC Uganda

Lweza FC waiangusha Vipers FC Uganda

Klabu ya soka ya Lweza FC, iliwaangusha mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka nchini Uganda Vipers FC kwa kuwafunga mabao 2 kwa 1 Jumanne jioni katika uwanja wa Wankulukuku jijini Kampala.

Mchuano huo ulitazamwa na maelfu ya mashabiki wa vlabu hivyo viwili nchini Uganda na kwingineko barani Afrika.

Kipindi cha kwanza, kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza hakuna klabu iliyokuwa imepata bao.

wadada_kalyowa-1132x509

Hata hivyo, Lweza FC ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia mchezaji wake Juma Bagala katika dakika ya 69 lakini mshambuliaji wa Uganda Cranes Erisa Ssekisambu aliisawazishia Vipers katika dakika ya 85 ya mchuano huo.

Emmanuel Kalyowa alikuwa shujaa wa Lweza baada ya kuipatia timu yake bao la ushindi katika dakika za ziada za mchuano wao na kufanya matokeo kuwa mabao 2 kwa 1 hadi mwisho wa mchuano huo.

Lweza sasa ni ya 12 kwa alama 16 huku Vipers ikisalia katika nafasi ya pili kwa 28.

Ligi inaongozwa na KCCA kwa alama 29, katika michuano 15 iliyochezwa katika ligi hiyo hadi sasa.

lweza_vipers_captains

Kikosi

Lweza F.C :
Charles Lukwago (G.K), Fred Okot, Nestroy Kizito, Mike Kabanda, Swaibu Mudde, Julius Mutyaba, Paddy Muhumuza, Fred Kalanzi (63′ Moses Ndawula), Juma Balinya (23′ Hassan Kikoyo), Emmanuel Kalyowa (80′ Geofrey Sserunkuma), Sula Bagala

Vipers SC :

Ismael Watenga (G.K), Nicolas Wadada (C), Aggrey Madoi, Halid Luwalira,Yusuf Mukisa, Deus Bukenya, Erisa Ssekisambu, Kezironi Kizito (51’Allan Kyambadde), Mike Mutyaba (61′ Mike Mutyaba), Ibrahim Saddam Juma (71′ Pius Wanji), Brian Nkuubi

Ligi hiyo itaendelea siku ya Ijumaa, URA itachuana na Maroons kuanzia saa 12 jioni.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in