Connect with us

CAF wateuawa waamuzi watakaochezesha vlabu vya DRC

CAF wateuawa waamuzi watakaochezesha vlabu vya DRC

 

Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limewateua marefarii kutoka Swaziland kuchezesha mchuano wa mzunguko wa kwanza kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika kati ya mabingwa watetezi TP Mazembe kutoka DRC na St.George ya Ethiopia.

Mchuano huo utapigwa katika uwanja wa Bahir Dar siku ya Jumapili.

Marefarii hao wataongozwa na Mbongiseni Fakudze Elliot atakayesaidiwa na Petros Mbingo Mzikayifani na Sifiso Nxumalo.

Tarehe 20 mwezi huu, Mazembe watakuwa nyumbani katika uwanja wao wa Stade TP Mazembe kurudiana na wapinzani wao.

Klabu nyingine, ya DRC inayoshiriki katika michuano hii, AS Vita Club, itakuwa nyumbani katika uwanja wa Tata Rafael kumenyana na Clube Ferroviario ya Msumbiji.

Waamuzi wa mchuano huu ni kutoka Eritrea wakiogozwa na Amanuel Eyob Russom na kusaidiwa na Angesom Obgamariam pamoja na Suleiman Ali Salih.

Katika taji la Shirikisho, klabu ya CS Don Bosco itakuwa Misri kuchuana na Misr Makkassa siku ya Jumamosi, mchuano utakaosimamiwa na refarii kutoka Somalia Hassan Mohamed Hagi.

Wawakilishi wengine wa DRC katika michuano hii FC St Eloi Lupopo,watakuwa wenyeji wa  El Ahly Shandy kutoka Sudan siku ya Jumapili katika uwanja wa Kibasa Maliba mjini Lubumbashi.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in