-
by
Victor Abuso
Shirikisho la soka nchini Sudan linadai kuwa timu ya taifa ya soka ya Kenya yenye vijana wasiozidi umri wa miaka 20, ilikuwa na wachezaji watano waliokuwa zaidi ya umri huo.
Hatua hii inakuja baada ya Kenya na Sudan kutoka sare ya bao 1 kwa 1 siku ya Jumapili wiki iliyopita jijini Khartoum, katika mchuano muhimu wa kusaka nafasi ya kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa itakayofanyika nchini Zambia mwaka ujao.
Mwekahazina wa Shirikisho hilo Oussama Ataelmaan, amesema kuwa Sudan itapeleka malalamisho yake kwa uongozi wa soka barani Afrika CAF.
Kanuni za CAF zinaweka wazi kuwa, ni wachezaji waliozaliwa baada January mwaka 1997 na baadaye ndio wanaoruhusiwa kushiriki katika mashidano hayo.
Sudan inasema kuwa wachezaji hao wa Kenya walizaliwa mwaka 1996.
Hata hivyo, rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya FKF Nick Mwendwa ametupilia mbali madai hayo na kusema wachezaji wote walichunguzwa kwa makini kabla ya mchuano huo.
Hii sio mara ya kwanza kwa Kenya kujipata katika hali hii, mwaka 2003, CAF iliIpiga marufuku Kenya kutoshiriki katika michuano ya vijana wasiozidi miaka 17 baada ya kubainika kuwa kulikuwa na wachezaji waliokuwa na umri mkubwa wakati huo na kuishinda Ghana mabao 3 kwa 2.
Mwaka 2014, Gambia ilifungiwa na CAF kwa miaka miwili kwa kosa hilo la kuwa na wachezaji wenye umri mkubwa katika timu yake ya timu ya vijana wasiozidi miaka 20.
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
CAF Champions League
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns Off to a Lukewarm Start in 2024/25 CAF Champions League
CAF Champions League
AL Ahly start CAF CL campaign with win over Stade d’Abidjan
CAF Confederation Cup
Simba make good start beating Bravos do Maquis
CAF Confederation Cup
Enyimba fall to Al Masry in Alexandria
CAF Confederation Cup
Zamalek got their Group D campaign off to a comfortable star
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...