-
-
by
Victor Abuso
Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limemfungua mchezaji wa AS Vita Club nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Emmanuel Ngudikama, kwa kutumia dawa za kusisimua misuli au kuomgeza nguvu mwilini wakati wa michuano ya Afrika CHAN iliyofanyika nchini Rwanda mapema mwaka huu.
Hata hivyo, CAF haijasema inamfungua mchezaji huyo kwa muda gani.
Ripoti kutoka katika Shirikisho la soka FECOFA, zinasema mchezaji huyo aligunduliwa kutumia dawa hiyo iliyopigwa marufuku na CAF baada ya mchuano wa nusu fainali kati ya DRC na Guinea.
Hii inaamanisha kuwa mchezaji huyo hatoshiriki katika michuano ya klabu yake na timu ya taifa ndani na nje ya nchi hiyo.
Ngudikama ni miongoni mwa wachezaji 23 walioisaidia DRC kunyakua ubingwa wa CHAN uliofanyika kati ya tarehe 16 mwezi Januari hadi Februari 8 nchini Rwanda.



CAF Confederation Cup
Simba book final spot in CAF Confederation cup

CAF Confederation Cup
Simba book final spot in CAF Confederation cup
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 5 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...