-
by
Victor Abuso
Michuano ya marudiano na ya mwisho kwa timu za taifa za soka kwa upande wa wanawake kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika itakayofanyika nchini Cameroon baadaye mwaka huu zinachezwa leo Jumanne.
Mataifa manane yatashiriki katika fainali hiyo itakayochezwa kati ya tarehe 19 Novemba hadi tarehe 3 mwezi Desemba katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo jijini Yaounde na Stade Municipal de Limbe mjini Limbe.
Tayari Cameroon ambao ni wenyeji wameshafuzu.
Mataifa mengine ambayo pia yamefuzu ni pamoja na mabingwa wa mwaka 2008 na 2012 Equitorial Guinea ambao wanashiriki kwa mara ya tano katika mashindano haya.
Misri ambayo inashiriki kwa mara ya pili nayo imeshafuzu pamoja na Zimbabwe ambayo haya ni makala yake ya nne kushiriki.
Mataifa manne yako mbioni kutafuta nafasi nne zinazosalia kucheza katika michuano hiyo ya kutafuta ubingwa wa Afrika.
Ratiba ya michuano ya leo Aprili 12 2016
- Kenya vs Algeria-Saa 9 mchana
- Nigeria vs Senegal-Saa 12 jioni
- Ghana vs Tunisia-Saa 12 Jioni
- Afrika Kusini vs Botswana-Saa 2 usiku
Mchuano wa Harambee Starlets ya Kenya na Algeria unasubiriwa sana na mashabiki wa soka nchini humo kwa sababu ikiwa Kenya itashinda, itashiriki katika michuano hiyo ya Afrika kwa mara ya kwanza.
Mechi ya kwanza ugenini warembo hao kutoka Kenya walilazimisha sare ya mabao 2 kwa 2 jijini Algers.
Mchuano huo utapigwa katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi na Shirikisho la soka nchini humo FKF limesema hakutakuwa na kiingilio ili mashabiki wafike kwa wingi kuishangilia timu yao.
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
CAF Champions League
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns Off to a Lukewarm Start in 2024/25 CAF Champions League
CAF Champions League
AL Ahly start CAF CL campaign with win over Stade d’Abidjan
CAF Confederation Cup
Simba make good start beating Bravos do Maquis
CAF Confederation Cup
Enyimba fall to Al Masry in Alexandria
CAF Confederation Cup
Zamalek got their Group D campaign off to a comfortable star
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...