Connect with us

Ulinzi na Tusker zafuzu nusu fainali TOP 8

Ulinzi na Tusker zafuzu nusu fainali TOP 8

 

Tusker FC na Ulinzi Stars zimefuzu katika hatua ya nusu fainali kuwania ubingwa wa taji la TOP 8 nchini Kenya.

Hii ni michuano ambayo huzikutanisha vlabu vinane vilivyomaliza katika nafasi nane bora msimu uliopita.

Vlabu hivyo ni pamoja na Bandari, Tusker, Ulinzi Stars, AFC Leopards, Gor Mahia, Ushuru, Sofapaka na Muhoroni Youth.

Tusker FC ilifuzu baada ya kuishinda Bandari FC kwa mabao 2 kwa 1, huku Ulinzi Stars ikiishinda AFC Leopards kwa mabao 3 kwa 2 katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi katika mechi zilizopigwa mwishoni mwa juma lililopita.

Siku ya Jumatatu, Gor Mahia wanachuana na Ushuru FC, huku Sofapaka wakipambana na Muhoroni Youth.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in