Connect with us

CAF 2016: Makundi ya klabu bingwa na Shirikisho yafahamika

CAF 2016: Makundi ya klabu bingwa na Shirikisho yafahamika

 

Hatimaye Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limeweka bayana hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa na Shirikisho mwaka huu wa 2016.

Mechi katika hatua hii zitachezwa nyumbani na ugenini na mshindi wa kwanza na wa pili watafuzu katika hatua ya nusu fainali.

Kuna makundi mawili, kila kundi na vlabu vinne kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika.

Hata hivyo, ilikuwa ni pigo kubwa kwa kalbu ya AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliyoondolewa katika michuano ya klabu bingwa baada ya kubainika kuwa mchezaji wake Idrissa Traore aliichezea klabu yake hata baada ya kupingwa marufu ya mechi minne wakati akiichezea klabu ya Stade Malien ya Mali.

Nafasi yake imechukuliwa na Mamelodi Sundowns ya Africa Kusini.

Michuano ya Klabu bingwa:-

Kundi A

Zesco United-Zambia

Al-Ahly-Misri

ASEC Mimosas-Cote Dvoire

Wydad Casablanca-Morroco

Kundi B

Enyimba-Nigeria

Zamalek-Misri

Es Setif-Algeria

Mamelodi Sundowns-Afrika Kusini.

Michuano ya kwanza itachezwa tarehe 17 mwezi Juni.

Michuano ya Shirikisho CAF:

Kundi A

MO Bejaia-Algeria

Young Africans-Tanzania

TP Mazembe-DRC

Medeama-Ghana

Kundi B

Kawkab Marrakech-Morroco

Etoile du Sahel-Tunisia

FUS Rabat-Morroco

Al-Ahli Tripoli-Libya.

Michuano ya kwanza itachezwa tarehe 17 mwezi Juni.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in