Connect with us

 

Michuano ya kimataifa ya kirafiki katika mchezo wa soka inaendelea leo barani Afrika na kwingineko duniani.

Kenya inacheza mechi ya pili baada ya kutoka sare ya bao 1 kwa 1 katika mchuano wa kwanza wa kirafiki mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Tanzania jijini Nairobi.

Harambee Stars inachuana na Falcons of Jediane ya Sudan katika mchuano wake huo wa pili katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi.

Kocha wa Kenya Stanley Okumbi ambaye ameongoza Harambee Stars katika michuano mitatu iliyopita, amefungwa mechi miwili na kutoka sare mechi moja na mchuano wa leo ni kipimo kwake kuona ikiwa atapata ushindi wake wa kwanza.

Kenya inatumia mchuano huu kujiweka tayari kumenyana na Congo Brazaville katika mchuano wa kufuzu kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Gabon.

Kenya tayari imeshaondolewa katika michuano hiyo na hakuna matumaini tena ya kusonga mbele.

Uganda nayo itakuwa nchini Zimbabwe kuchuana na Warriors katika uwanja wa Rufaro jijini Harare.

Cranes nayo inatumia mechi hii kujiweka kumenya na Bostwana ugenini tarehe 4 mwezi Juni kutafuta nafasi ya kucheza fainali ya mataifa bingwa barani Afrika.

Kikosi cha Uganda: Dennis Onyango and Robert OdongkaraDenis Iguma, Joseph Ochaya, Wasswa Hassan Mawanda, Juuko Murushid, Isaac Isinde, William Luwagga Kizito, Godfrey  Walusimbi, Aucho Khalid, Yassar Mugerwa, Tony MawejjeEmmanuel Okwi, Erisa Ssekisambu, Davis Kasirye, Geofrey Massa, Faruku Miya, Lorenzen Melvyn na Edris Lubega.

Matokeo ya jana Mei 30 2016:-

Gambia 0 vs Zambia 0

Ufaransa 3 vs Cameroon 2.

More in