Connect with us

 

Zesco United ya Zambia ilishindwa kuhimili uzoefu ya Wydad Casablanca ya Morroco ugenini na kufungwa mabao 2 kwa 0 katika mchuano wao wa pili hatua ya makundi, kuwania taji la klabu bingwa barani.

Mchuano huo ulichezwa Jumatano usiku katika uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat.

Wydad Casablanca ilipata bao lake la kwanza kupitia El Karti katika dakika ya 13 kipindi cha kwanza cha mchuano huo, huku bao la pili likawa la kujifunga kutoka kwa beki wa Zesco United George Owino katika dakika ya 51 kipindi cha pili.

Kwa matokeo haya, Wydad Casablanca inaongoza kundi la A kwa alama 6, ikifuatwa na ASEC Mimosas ya Ivory Coast iliyoifunga Al-Ahly ya Misri mabao 2 kwa 1 siku ya Jumanne.

Zesco United ni ya tatu pia kwa alama 3 huku Al-Ahly ikiwa ya mwisho bila ya alama yoyote.

Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, ilisahau masaibu ya wiki moja iliyopita baada ya kufutwa kwa ushindi wake dhidi ya ES Setif iliyofungwa wiki moja iliyopita, na kuifunga Enyimba ya Nigeria kwa mabao 2 kwa 1.

Mamelodi Sundowns na Zamalek FC wana alama tatu katika kundi hili la B.

Meadama FC ya Ghana ikicheza nyumbani dhidi ya MO Bejaia, katika mechi ya kundi A, katika taji la Shirikisho, ilitoka sare ya kutofungana.

Matokeo hayo yanaiweka MO Bejaia katika nafasi ya pili kwa alama 4, nyumba ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayoongoza kwa alama 6.

Sare nyingine, pia ilikuwa katika mechi ya kundi B kati ya Etoile du Sahel na FUS Rabat, ilitoka sare ya bao 1 kwa 1.

Kundi hili linaongozwa na Kawkab Marrakech ya Morroco kwa alama 6 ikifuatwa na FUS Rabat ya pia kutoka Morroco kwa alama 4.

Mechi zijazo zitachezwa mwishoni mwa mwezi Julai.

More in