Connect with us

Klabu ya soka ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tayari imejikatia tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali kuwania taji Shirikisho barani Afrika baada ya kuandikisha ushindi muhimu wa bao 1 kwa 0 dhidi ya MO Bejaia ya Algeria.

Mchuano huo ulichezwa mjini Lubumbashi wiki hii, na sasa Mazembe inaongoza kundi la A kwa alama 10 baada ya kucheza mechi nne.

Medeama FC ya Ghana na MO Bejaia ambazo zina alama tano, zinasubiri mechi za mwisho ili kufahamu atayejiunga na Mazembe katika hatua ya nusu fainali.

Nayo Yanga FC ya Tanzania ambayo ilifika katika hatua hii kwa mara ya kwanza, inamaliza vibaya baada ya kupoteza mechi zake zote nne, ni ya mwisho bila ya alama yoyote.

Wawakilishi hawa wa Tanzania na Afrika Mashariki, sasa wanasubiri michuano ya mwisho dhidi ya MO Bejaia nyumbani tarehe 13 mezi ujao na baadaye kumaliza na TP Mazembe mjini Lububashi baadaye mwezi ujao angalau kupata ushindi.

Kundi B, FUS Rabat inaelekea kufuzu baada ya kuendelea kuongoza kundi hili kwa alama 10.

Klabu hii kutoka nchini Morocco imeshinda mechi tatu kati ya nne ilizocheza na wiki hii iliishinda Kawkab Marrakech pia kutoka Misri kwa mabao 3-1.

Etoile du Sahel kutoka Tunisia ni ya pili kwa alama 7 nyuma ya Kawkab Marrakech ambayo ni tatu kwa alama 6.

Al-Ahli Tripoli ya Libya ambayo tayari imeondolewa katika michuano hii, imefungwa mechi zao zote hadi sasa na haina alama yoyote.

More in