Michuano ya soka kuwania medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki kwa upande wa wanaume na wanawake, inaaza kutifua vumbi tarehe 3 mwezi ujao nchini Brazil.
Mataifa 16 kwa upande wa wanaume na 12 kwa upande wa wanawake kutoka mabara 6 kote duniani yanashiriki katika michuano hii itakayomaliza tarehe 20 mwezi Agosti.
Viwanja saba vitatumiwa kuandaa michezo hii huku mchuano wa ufunguzi ukiwa ni katii ya Sweden na Afrika Kusini, lakini baadaye wenyeji Brazil na China kwa upande wa wanawake.
Kwa upande wa timu ya wanaume, wenyeji Brazil watafugua dimba dhidi ya Afrika Kusini, huku Iraq ikimenyana na Denmark siku ya Alhamisi.
Kuna makundi manne katika michuano ya wanaume, huku timu za wanawake zikigawanywa kwa makundi matatu.
Afrika Kusini na Zimbabwe zinawakilisha bara la Afrika upande wa wanawake katika michuano hii.
Banyana Banyana imejumuishwa katika kundi moja na Brazil, Sweden na China huku The Mighty Warriors ya Zimbabwe ikiwa pamoja na Canada, Australia na Ujerumani.
Mwaka 2012, bara la Afrika liliwakilishwa na Senegal, Gabon na Morocco kwa upande wa wanaume huku Cameroon na Afrika Kuisni zikiwakilisha wanaume.
Mabingwa watetezi ni Mexico kwa upande wa wanaume na Marekani kwa upande wa wanawake.
Mshindi katika kila kundi, na atakayemaliza katika nafasi ya pili atafuzu katika hatua ya robo fainali.
Bara la Afrika linawakilishwa na mataifa matatu Algeria, Nigeria na Afrika Kusini na hivi vikosi vya wachezaji wasiodizi miaka 23.
Afrika Kusini imepangwa katika kundi la A pamoja na Brazil, Iraq na Denmark.
Nigeria ipo katika kundi B pamoja na Sweden, Colombia na Japan, huku Algeria ikipangiwa Honduras, Ureno na Argentina.