Timu ya taifa ya soka ya Nigeria yenye wachezaji wenye chini ya miaka 23, wamefanikiwa kufuzu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Olimpiki inayoendelea nchini Brazil.
Super Eagles imefuzu katika hatua hii baada ya kuifunga Sweden bao 1 kwa 0 katika mchuano wake wa pili wa hatua ya makundi.
Bao hilo la pekee la Nigeria lilifungwa na Sadiq Umar.
Nigeria ilianza vizuri kutafuta ubingwa wake wa pili baada ya kuifunga Japan mabao 5 kwa 4 katika mchuano wa kwanza.
Mechi ya mwisho ya kutamatisha hatua ya makundi itakuwa dhidi ya Colombia siku ya Jumanne.
Mwaka 1996, wakati michezo hii ilipoandaliwa nchini Marekani, Nigeria walinyakua taji hilo.
Wawakilishi wengine wa bara Afrika, Afrika Kusini matumaini ya kusonga mbele yamedidimia baada ya kufungwa na Denmark bao 1 kwa 0 na kutoka sare ya kutofungana na wenyeji Brazil katika mchuano wa ufunguzi.
Mechi ya mwisho itakuwa ni dhidi ya Iraq.
Algeria nayo imeondolewa baada ya kufungwa michuano yote miwili dhidi ya Argentina mabao 2 kwa na Honduras mabao 3 kwa 2.
Mechi ya kumaliza makundi itakuwa dhidi ya Ureno.
Kwa upande wa wanawake, wawakilishi wa Afrika kuelekea kumaliza mechi za makundi kesho wameondolewa katika michuano hii.
Zimbabwe dhidi ya Australia na Afrika Kusini dhidi ya wenyeji Brazil.