Connect with us

 

Shirikisho la soka nchini Congo Brazaville limemfuta kazi kocha wa timu ya taifa Pierre Lechantre miezi 17 kabla ya mkataba wake kumalizika.

Uongozi wa soka nchini humo umesema umezungumza na kocha huyo na kuafikiana naye kuwa aache kazi baada ya matokeo mabaya ya kufuzu kushiriki kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Matokeo mabaya ya hivi karibuni ya Congo Brazaville yalikuwa dhidi ya Uganda baada ya kufungwa bao 1-0 jijini Kampala mwishoni mwa wiki iliyopita.

miya_celebration-1132x509

Lechantre alipewa kibarua cha kukinoa kikosi hicho baada ya kuchukua nafasi ya Mfaransa mwenzake Claude LeRoy.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 66, kabla ya kuifunza Congo Brazaville aliwahi pia kuifunza Cameroon na Mali.

Congo Brazaville sasa inamtafuta kocha mpya, kuanza kuiandaa kikosi hicho kabla ya kumenyana na Ghana katika mchuano mwingine dhidi ya Ghana mwezi Agosti mwaka ujao.

Congo haina alama katika kundi lao pamoja na Misri, Ghana na Uganda.

More in