Michuano ya soka inayochezwa ufukweni kuwania taji la bara Afrika inaanza siku ya Jumanne jijini Lagos nchini Nigeria.
Mataifa nane yanashiriki katika michuano hii huku timu mbili zitakafika katika hatua ya fainali, zitafuzu katika michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwezi Aprili mwaka ujao nchini Bahamas.
Mwaka 2015, michuano hii ilifanyika Visiwani Ushelisheli na Madgascar wakaibuka mabingwa.
Mataifa yanayoshiriki ni pamoja na:- Wenyeji Nigeria, Misri,Ghana,Ivory Coast, Libya, Madagascar,Morocco na Senegal.
Kundi la A: Nigeria, Misri, Ghana na Ivory.
Kundi B: Madagascar, Libya, Morocco na Senegal.
Ratiba Desemba 13 2016:-
- Ghana vs Ivory Coast
- Nigeria vs Misri
- Madagascar vs Libya
- Morocco vs Senegal