Connect with us

 

Kiungo wa klabu ya soka ya Western Stima Kenneth Muguna ndio mchezaji bora na mwenye thamani kubwa mwaka 2016 nchini Kenya.

Kiungo huyo wa Kati, alipata tuzo hiyo siku ya Jumanne usiku jijini Nairobi na kumshinda Eric Ouma wa Gor Mahia na Humfrey Mieno wa Tusker FC.

Licha ya kuwa mchezaji bora, Muguna alipata tuzo ya kiungo bora wa mwaka na kuzawadiwa Shilingi za Kenya Millioni 1.5.

Taji la kocha bora wa mwaka, lilimwendea Paul Nkata wa Tusker FC, baada ya kuiongoza klabu hiyo kushinda taji la msimu huu nchini humo.

Nkata raia wa Uganda, aliwashinda makocha wengine Ze Maria wa Gor Mahia na Francis Baraza kutoka Chemelil Sugar FC.

Orodha Kamili

Kipa bora wa mwaka:

Patrick Matasi – Posta Rangers

Beki bora

Jockins Atudo – Posta Rangers

Kiungo bora wa Kati

Miguna Kenneth – Western Stima

Mfungaji bora

John Makwata – Ulinzi Stars

Mchezaji bora wa mwaka 2016

Eric Ouma – Gor Mahia

More in