Connect with us

Wachezaji wa timu ya soka ya wanawake wa Nigeria, wameandamana nje ya majengo ya bunge jijini Abuja, kulalamikia hatua ya Shirikisho la soka nchini humo NFF kutowalipa marupurupu yao.

Kikosi hicho ambacho hivi maajuzi kilishinda taji la nane la mataifa bingwa barani Afrika nchini Cameroon, mbali na maandamano hayo, kimekataa kuondoka Hotelini jijini Abuja hadi pale watakapolipwa fedha zao.

Kila mchezaji wa Super Falcons, analidai Shirikisho nchini humo Dola za Marekani 23,650 ahadi waliyopewa kabla ya kwenda kushiriki michuano ya bara Afrika.

Maandamano haya yamekuja wakati huu rais Muhamadu Buhari akihudhuria vikao vya bunge hivi leo kuwasilisha Bajeti ya fedha ya mwaka 2017.

Haya ni baadhi ya maandishi katika mabango ya wachezaji hao , “Sisi ni watoto wako, tuonee huruma”,.”Tuwaheshimu wanawake,”. ”Wachezaji wakike wanahitaji kuheshimiwa.”

Uongozi wa soka nchini Nigeria unasema unaelewa malalamishi ya wachezaji hao lakini hauna fedha za kuwalipa.

More in