Gabon imekuwa timu ya kwanza kutaja kikosi chake cha mwisho kitakachoshiriki katika fainali ya michuano ya Mataifa bingwa barani Afrika itakayoanza tarehe 14 mwezi Januari.
Michuano hii itafanyika nchini Gabon na serikali inasema maandalizi yote yamekamilika.
Kikosi hicho cha kocha José Antonio Camacho, kinaongozwa na nahodha Pierre-Emerick Aubameyang anayechezea klabu ya Borrusia Dortmund nchini Ujerumani.
Kiungo wa Kati Didier Ndong, anayecheza katika klabu ya Sunderland nchini Uingereza, amejumuishwa katika kikosi hicho baada ya kuachwa katika mchuano muhimu wa kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Mali mwezi Novemba.
Wachezaji wengine waliojumuishwa katika kikosi hicho ni pamoja na kiungo wa Kati wa klabu ya Juventus Mario Lemina, Bruno Ecuélé Manga kutoka klabu ya klabu ya Cardiff City na mshambuliaji Malick Evouna anayecheza soka nchini China.
Mchuano wa ufunguzi utakuwa dhidi ya Guinea Bissau tarehe 14 mwezi Januari katika michuano ambayo itamalizika tarehe 5 mwezi Februari.
Gabon wamepangwa katika kundi la A na mabingwa mara nne wa michuano hii Cameroon na Burkina Faso waliofika katika hatua ya fainali ya mwaka 2013.
Kikosi kamili cha Gabon:
Makipa: Didier Ovono (Oostende, Ubelgiji), Yves Stéphane Bitséki Moto (CF Mounana), Anthony Mfa Mezui (Hana klabu).
Mabeki: Lloyd Palun (Red Star, Ufaransa), André Biyogho Poko (Karabukspor, Uturuki), Aaron Appindangoye (Stade Lavallois, Ufaransa), Franck Perrin Obambou (Stade Mandji), Bruno Ecuélé Manga (Cardiff City, Wales), Yoann Wachter (CS Sedan Ardennes, Ufaransa), Johann Serge Obiang (Troyes, Ufaransa), Benjamin Zé Ondo (Mosta FC, Malta)
Viungo wa Kati: Mario René Junior Lemina (Juventus, Italia), Junior Serge Martinsson Ngouali (IF Brommapojkarna, Sweden), Levy Clément Madinda (Gimnàstic, Uhispania), Guélor Kanga Kaku (Red Star Belgrade, Serbia), Merlin Tandjigora (Meixian Hakka FC, China), Didier Ibrahim Ndong (Sunderland, Uingereza), Samson Mbingui (Raja Casablanca, Morocco)
Washambuliaji: Pierre Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund, Ujerumani), Malick Evouna (Tianjin Teda FC, China), Denis Athanase Bouanga (Tours, Ufaransa), Serge Kevyn Aboue Angoue (Uniao Leiria, Ureno), Cedric Ondo Biyoghe (CF Mounana)
Wachezaji wa ziada: Axel Meyé (Eskisehirspor, Uturuki), Johan Lengoualama (Raja Casablanca, Morocco), Donald Nzé (AS Pelican)