Connect with us

Timu ya taifa ya soka ya Uganda inakabiliwa na changamoto za kifedha kuelekea kwenye michuano ya Mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

 Uganda imefuzu katika michuano hii kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978.

Shirikisho la soka nchini humo FUFA, linasema  linasubiri msaada wa fedha ili kusaidia  kukiandaa kikosi hicho cha taifa.

Uganda Cranes inahitaji Dola za Marekani Milioni 2.1 kufanakisha maandalizi yake ikiwa ni pamoja na kwenda kupiga kambi nchini Tunisia na Dubai.

Mbali na fedha hizo kusaidia katika maandalizi, wachezaji na kocha watahitaji kulipwa marupurupu yao wakiwa kambini na wakati wakishiriki katika michuano hiyo.

Uganda imepangwa katika kundi D pamoja na Misri, Ghana na Mali.

Ratiba ya maandalizi:

  • Januari 4: Tunisia vs. Uganda
  • Januari 8: Slovakia vs. Uganda
  • Januari 11: Ivory Coast vs. Uganda

Ratiba ya michuano ya hatua ya makundi kundi D, michuano ya AFCON:

  • Januari 17: Ghana vs. Uganda
  • Januari 21: Egypt vs. Uganda
  • Januari 25: Uganda vs. Mali

Makundi ya michuano ya AFCON:

Kundi A: Gabon, Burkina Faso, Cameroon, Guinea Bissau
Kundi B: Algeria, Senegal, Tunisia, Zimbabwe
Kundi C: Ivory Coast, DR Congo, Morocco, Togo
Kundi D: Ghana, Mali, Egypt, Uganda

More in