DR Congo
Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maarufu kama Leopard, inarejea katika michuano ya kutafuta ubingwa wa Afrika kwa mara ya 16.
Mara ya kwanza kwa DRC kushiriki katika michuano hii mikubwa barani Afrika, wakati huo ikiwa inaitwa Zaire, ilikuwa ni mwaka 1965.
Mwaka 2015,ndio mara ya mwisho kwa nchi hii kushiriki katika michuano hii ilipofanyika nchini Equatorial Guinea na kumaliza katika nafasi ya tatu.
Safari ya kwenda Gabon
Mabingwa walioshinda taji hili mara mbili, mwaka 1968 na 1974, walimaliza wa kwanza katika kundi lao la B walilopangwa na Angola, Madagascar na Jamhuri ya Afrika ya Kati, kutafuta tiketi ya kwenda Gabon.
Nchini Gabon, Leopard ambayo ni ya 48 duniani, imepangwa katika kundi moja la C na mabingwa watetezi Ivory Coast, Morocco na Togo.
Leopard inatumai kuwa itamaliza katika mbili bora ili kufuzu katika hatua ya mwondoano na kutafuta ubingwa ambao mara ya mwisho walishinda miaka 42 iliyopita.
Kocha
DR Congo inafuzwa na Florent Ibenge mwenye umri wa miaka 55, na ni miongoni mwa makocha wanne pekee wa nyumbani wanaofunza mataifa yao.
Makocha wengine wa nyumbani wanaofunza nchi zao ni kutoka Zimbabwe, Guinea Bissau na Senegal.
Ibenge alianza kuifunza Leopard mwezi Agosti mwaka 2014, baada ya kuchukua nafasi ya raia mwenzake Jean Santos Muntubilla.
Atakumbukwa kuiongoza DRC kushinda taji la Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN mwaka 2016, michuano iliyofanyika nchini Rwanda.
Kikosi
Kikosi cha sasa cha Leopard kinawajumuisha wachezaji wengi walioshinda taji la CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani ,akiwemo kipa wa klabu ya TP Mazembe Ley Matampi, Issama Mpeko, Merveille Bokadi, Jonathan Bolingi, Elia Meschak na Joyce Lomalisa.
Hata hivyo, Ibenge itamkosa mchezaji wa Everton Yannick Bolasie, ambaye anauguza majeraha.
Kikosi kamili:
Makipa: Kiassumbua Joel (whollen fc/ suisse), Matampi Vumi Ley (TP Mazembe/ RD Congo), Kudimbana Nicaise (Antwerp/ Ubelgiji)
Mabeki: Issama Mpeko Djo (TP Mazembe/ RD Congo), Bope Bokadi Merveille (TP Mazembe/ RD Congo), Lomalisa Mutambala (AS V.Club/ RD Congo), Ikoko Jordan (Guingamp/ Ufaransa), Tisserand Marcel (Fc Ingolstadt/ Ujerumani), Zakuani Gabriel (Peterborough/ Uingereza), Fabrice N’sakala (Alanyaspor/ Uturuki)
Viungo wa Kati: Mulumba Remy (Gazele Fc Ajaccio/ Ufaransa), Mpoku Paul-Jose (Panathinaikos/ Ugiriki), Herve Kage (Kv Courtrai/ Ubelgiji), Mbemba Chancel (Newcastle/ Uingereza), Youssuf Mulumbu (Norwich City/ Uingereza), Maghoma Jacques (Birmingham/ Uingereza), Kebano Neeskens (Fulham/ Uingereza)
Washambuliaji: Mubele Ndombe Firmin (Al Ahli Doha/ Qatar), Junior Kabananga (Astana / Kazakhstan), Jeremy Bokila Loteteka (Al Quarittyah/ Qatar), Bakambu Cedrick (Villareal/ Uhispania), Bolingi Mpangi Jonathan (Tp Mazembe/ DRC), Botaka Jordan (Charlton/ Uingereza), Mbokani Bezua Dieumerci (Hull City/ Uingereza)
Maandalizi
Leopard inapiga kambi nchini Cameroon ikisubiri mchuano wake wa ufunguzi dhidi ya Morocco katika uwanja wa d’Oyem tarehe 16 Januari.
IVORY COAST
Ivory Coast au Cote Dvoire, ndio mabingwa watetezi wa taji hili, waliloshinda mwaka 2015 nchini Equitorial Guinea baada ya kusubiri kwa muda mrefu tangu 1992.
Haya ni makala ya 22 ya michuano hii katika historia yake ya michuano hii ya mataifa bingwa.
Safari ya kwenda Gabon
The Elephants kama wanavyofahamika kwa jina la utani, walifuzu katika michuano hii, baada ya kushinda kundi la I kwa alama 6, nyuma ya Sierra Leone iliyomaliza kwa alama 5 huku Sudan ikiwa ya mwisho kwa alama 4.
Hili ni kundi ambalo lilitoa mshindi mmoja kwa sababu kulikuwa tu na mataifa matatu, yaliyoshiriki katika michuano hii ya kufuzu.
Kocha
Ivory Coast inafunzwa na Mfaransa Michel Dussuyer.
Kabla ya kupewa kibarua nchini Ivory Coast, alikuwa anaifunza timu ya taifa ya Guinea kati ya mwaka 2010-2013 na baadaye mwaka 2014-2015.
Kocha huyu mwenye umri wa miaka 57, amewahi pia kuifunza Benin kati ya mwaka 2008-2010.
Nchi yake ya kwanza kuifunza ilikuwa ni Guinea mwaka 2002.
Ni kocha ambaye ametumia kuifunza Guinea kwa muda wa miaka 7.
Kikosi
Ivory Coast inajivunia na wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa katika mataifa mengi ya bara Ulaya. Ni kikosi cha wachezaji wanaotajwa kuwa na vipaji vya hali ya juu.
Hata hivyo, Yao Gervinho atakosa michuano ya mwaka huu kwa sababu ya jeraha la goti analouguza na anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi sita.
Yaya Toure mchezaji wa Manchester City yeye amestaafu kucheza soka la Kimataifa.
Hiki ndiko kikosi kamili:
Makipa: Sylvain Gbohouo (TP Mazembe/COD), Ali Badra Sangare (Tanda), Mande Sayouba (Stabaek/NOR)
Mabeki: Serge Aurier (PSG/Ufaransa), Mamadou Bagayoko (Saint-Trond/UBELGIJI), Eric Bailly (Manchester Utd/UINGEREZA), Simon Deli (Slavia Prague/CZECH), Ousmane Viera Diarrassouba (Adanaspor/UTURUKI), Wilfried Kanon (ADO Hague/Uholanzi), Lamine Kone (Sunderland/Uingereza), Adama Traore (Basel/Uswizi)
Viungo wa Kati: Victorien Angban (Granada/Uhispania), Geoffrey Serey Die (Basel/Uswizi), Cheick Doukoure (Metz/Ufaransa), Franck Kessie (Atalanta Bergamo/Italia), Yao Serge N’Guessan (Nancy/Ufaransa), Jean-Michaël Seri (Nice/Ufaransa)
Washambuliaji: Wilfried Bony (Stoke City/Uingereza), Max-Alain Gradel (Bournemouth/Uingereza), Salomon Kalou (Hertha Berlin/Ujerumani), Jonathan Kodjia (Aston Villa/Uingereza), Nicolas Pepe (Angers/Ufaransa), Giovanni Sio (Rennes/Ufaransa), Wilfried Zaha (Crystal Palace/Uingereza).
Maandalizi
Kikosi cha Ivory Coast kinapiga kambi mjini Abu Dhabi, katika Falme za kiarabu.
Serikali ya Ivory Coast ilitoa Euro Milioni 6 kusaidia maandalizi ya kikosi hiki kutoka Euro 600,000 kama ilivyokuwa miaka miwili iliyopita nchini Equitorial Guinea walikopata ushindi.
Kuelekea katika michuano hii imepangwa kucheza na Uganda na Sweden katika mchuano wa maandalizi.
Morocco
The Atlas Lions ni timu nyingine katika kundi hili la C.
Mabingwa hawa wa mwaka 1976, wanashiriki katika michuano hii kwa mara 16.
Mara ya mwisho kwa Atlas Lions kushiriki katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 2013 nchini Afrika Kusini na kuondolewa katika hatua ya makundi.
Safari ya kwenda Gabon
Morocco ilimaliza wa kwanza la kundi la F kwa alama 16 katika michuano ya kufuzu kwenda nchini Gabon.
Baada ya michuano sita, ilishinda mechi tano nyumbani na ugenini na kwenda sare mchuano mmoja ilipotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Libya.
Morocco imepangwa katika kundi la C na Togo, Ivory Coast na DRC.
Mwaka 2013, iliondolewa katika hatua ya makundi na inatumai kuwa mwaka huu mambo yatakwenda vizuri.
Kocha
Kocha wa sasa wa Morocco ni Mfaransa, Herve Renard.
Alianza kuifunza timu hiyo mwaka 2016.
Mwaka 2015 akiifunza Cote Dvoire, aliisaidia kushinda taji la AFCON baada ya kusubiri kwa muda mrefu.
Mwaka 2012 akiifunza Zambia, aliiongoza kunyakua taji lake la kwanza wakati michuano hii ilipofanyika nchini Gabon.
Renard mwenye umri wa miaka 28, ambaye anajivunia rekodi nzuri barani Afrika Afrika, mwaka 2010 aliwahi pia kocha wa Angola lakini pia klabu ya USM Alger mwaka 2011 nchini Algeria.
Kikosi
Makipa : Munir Kajoui (Numancia/ESP), Yassine Bounou (Girona/ESP), Yassine Kharroubi (Lokomotiv Plodviv/BUL).
Mabeki: Mehdi Benatia (Juventus/Italia ), Marouane Da Costa (Olympiakos/Ugiriki), Amine Attouchi (Wydad Casablanca), Fouad Chafik (Dijon/Ufaransa), Hamza Mendil (Lille/Ufaransa), Nabil Dirar (Monaco/Ufaransa), Romain Saiss (Wolverhampton/Uingereza).
Viungo wa Kati: Mounir Obbadi (Lille/Ufaransa), Karim El Ahmadi (Feyenoord/Uholanzi), Youssef Ait Bennasser (Nancy/Ufaransa), Mbarek Boussoufa (El Jazira/Falme za Kiarabu, Fayçal Fajr (Deportivo La Corogne/Uhispania), Noureddine Amrabat (Watford/Uingereza), Soufiane Boufal (Southampton/Uingereza), Mehdi Carcela (Granada/Uhispania).
Washambuliaji: Youssef El Arabi (Lekhwiya/Qatar), Youssef Ennesyri (Malaga/Uhispania), Khalid Boutayeb (Strasbourg/Ufaransa), Rachid Alioui (Nimes/Ufaransa), Aziz Bouhaddouz (St Pauli/Ujerumani).
Maandalizi
The Atlas Lions inapiga kambi katika Falme za kiarabu.
Itacheza mechi mbili za Kimataifa dhidi ya Iran na Finland kabla ya kwenda nchini Gabon.
Togo.
Les Eperviers , au The Sparrow Hawks, inashiriki katika michuano hii kwa mara ya nane.
Mara ya mwisho kucheza katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 2013 wakati fainali hii ilipochezwa nchini Afrika Kusini na kufika katika hatua ya robo fainali.
Ilianza kucheza katika michuano hii mwaka 1972.
Safari ya kwenda Gabon
Togo ilikuwa katika kundi moja na Tunisia, Liberia na Djibouti katika michuano ya kufuzu kucheza fainali hii.
Kati ya mechi 6 ilizocheza, ilishinda mechi tatu, kwenda sare mabara mbili na kufungwa mara moja.
Ilifuzu kama mojawapo ya timu bora iliyomaliza katika nafasi ya pili katika michuano hii.
Kocha
Kocha wa Togo ni Mfaransa Claude le Roy.
Le Roy mwenye umri wa miaka 68, ambaye ana historia ya kipekee kufunza soka kwa muda mrefu barani Afrika, alijiunga na Togo mwaka 2016.
Mbali na Togo, amewahi kuwa kocha wa Congo Brazaville kati ya 2013-2015, DR Congo 2011-2013, Ghana 2006-2008, DR Congo 2004-2006, Cameroon 1998, 1985-1988, Senegal 1989-1992.
Kikosi
Makipa: Kossi Agassa (Hana Klabu), Cedric Mensah (Le Mans/Ufaransa), Baba Tchagouni (Marmande/Ufaransa)
Mabeki: Serge Akakpo (Trabzonspor/Uturuki), Vincent Bossou (Young Africans/Tanzania), Djene Dakonam (Saint-Trond/Belgium), Joseph Douhadji (Rivers Utd/Nigeria), Maklibe Kouloun (Dyto), Gafar Mamah (Dacia/MDA), Sadate Ouro-Akoriko (Al Khaleej/KSA), Hakim Ouro-Sama (Port)
Viungo wa Kati: Lalawele Atakora (Helsingborgs/Sweden), Franco Atchou (Dyto), Floyd Ayite (Fulham/Uingereza), Ihlas Bebou (Fortuna Dusseldorf/Ujerumani), Matthieu Dossevi (Standard Liege/Ubelgiji), Henritse Eninful (Doxa/Ujerumani), Serge Gakpe (Genoa/Italia), Victor Nukafu (Entente II), Alaixys Romao (Olympiacos/Ugiriki, Prince Segbefia (Goztepe/Uturuki)
Washambuliaji: Emmanuel Adebayor (Hana klabu, capt), Komlan Agbeniadan (WAFA/Ghana), Razak Boukari (Chateauroux/Ufaransa), Fo Doh Laba(Berkane/Morocco)
Maandalizi
Kikosi cha Togo, kiliwasili nchini Senegal kwa usafiri wa ndege ya rais Faure Gnassingbe, kwa maandalizi ya michuano hii muhimu kabla ya kwenda nchini Gabon.
Togo imepangwa pamoja na Cote d’Ivoire, DR Congo na Morocco.