Connect with us

Moses Basena:Soka la Afrika Mashariki linafanana

Moses Basena:Soka la Afrika Mashariki linafanana

Na Victor Abuso,

Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya soka ya Uganda na klabu ya Simba Uganda, Moses Basena anasema kiwango cha soka katika nchi za Afrika Mashariki kinafanana na ni sababu mojawapo ya kutofika mbali katika michuano ya Kimataifa.

Akizugumza na Soka25east.com, Basena amesema tofauti inayoweza kushuhudiwa tu ni namna vlabu mbalimbali vinavyowania ubingwa wa ligi nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi.

Basena ambaye amewahi kuwa kocha wa Simba Tanzania, SC Villa, URA FC, Express FC zote za Uganda amesema :-

“Kwa uozefu wangu kama kocha na ninavyoona hali ya soka hapa kwetu Afrika Mashariki na Kati, kiwango ni kile kile na makocha wanastahili kubadilisha mbinu wanazotumia ili kubadilisha mambo,”.

Hata hivyo, Basena amedokeza kuwa kidogo nchini Uganda ligi kuu ya soka ina ushindani mkubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine katika eneo hilo kwa sababu mechi nne au tatu kabla ya kumalizika kwa ligi mara nyingi ni vigumu kufahamu ni nani atakayeshinda ligi.

Mabingwa wa mwaka huu Vipers FC walilazimika kusubiri mchuano wao wa mwisho kujihakikishia ubingwa msimu huu.

Nchini Kenya, Basena anasema licha ya ushindani kuwepo, kwa mtazamo wake ni klabu moja tu ndio inayotupiwa macho ambayo ni Gor Mahia.

Gor Mahia ni mabingwawa soka nchini humo na wamenyakua ligi mara mbili mfululizo na wakati huu wapo katika harakati za kutetea taji lake.

“Lakini kitu kingine ninachokiona kuhusu wachezaji wa Kenya, hawana uwezo wa kustahimili misuli.Wanachoka sana. Hivyo ndivyo nionavyo,”.

Kuhusu Tanzania, Basena kwa thathmini akiwa kocha wa zamani wa klabu ya Simba, anaona kuwa ushindani ni kati ya vlabu vitatu ambavyo ni mabingwa wa msimu hu Yanga, Simba FC na sasa Azam.

Basena anasisitiza kuwa wachezaji wa Tanzania hawana nidhamu nje ya uwanja.

‘Tatizo la wachezaji wa Tanzania ni kukosa nidhamu wanapokuwa uwanjani, hali hii inarudisha nyuma kiwango cha soka nchini humo,”.

Wachezaji nchini Tanzania wamekuwa wakilalamikiwa kuwa ni watu wanaopenda kujiburudisha mno baada ya mechi unawakuta baa wakinywa pombe ilhali siku inayofutia wana mechi na wengine wanadaiwa kuwa na zaidi ya mpenzi mmoja suala ambalo linawaathiri mno.

Pamoja na hayo, amewasifu sana watanzania kwa kuonesha mapenzi makubwa ya soka kwa namna wanapofurika uwanjani wakati wa michuano ya ligi kinyume na ilivyo nchini Uganda na Kenya.

Suala lingine ambalo anaona linastahili kufanyiwa kazi ni kwa makocha Afrika Mashariki kuwapa mafunzo sahihi wachezaji wao ili wanapokwenda katika nchi za kigeni mfano Ulaya waoneshe kiwango cha hali ya juu kinyume na hali ilivyo sasa.

 

 

 

 

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in