Na Victor Abuso,
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Adel Amrouche ambaye pia anajulikana kwa jina ya utani kama “Msanifu” anatajwa kuwa miongoni mwa makocha wanaopewa kipau mbele ya kuchukua nafasi ya kocha wa Tanzania Mart Nooij.
Duru kutoka Dar es salaam zimeimbia soka25east.com kuwa kutokana na matokeo mabaya katika michuano ya Kusini mwa Afrika COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini huenda ndio ikawa nafasi ya mwisho kocha huyo kuifunza Tanzania.
Nooij raia wa Uholazni alijiunga na Taifa Stars mwaka 2014 na kuchukua nafasi ya Kim Poulsen aliyefutwa kazi kutokana na matokeo mabaya ya michuano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA mwaka 2013.
Katika michuano mitatu iliyopita, Taifa Stars imeshindwa kupata ushindi hali inayoweka kibarua cha Nooij hatarini.
Hasira za wapenzi wa soka nchini Tanzania zimedhirishwa kutokana na majibizano yanyoendelea kupitia mitandano ya kijamii kumshinikiza Nooij kufutwa kazi.
Tayari uongozi wa TFF chini ya rais wake Jamal Malinzi umesema kuwa utachukua hatua kuhakikisha kuwa kiwango cha soka kinapanda baada ya matokeo mabaya nchini Afrika Kusini.
Tanzania imefungwa katika michuano yake miwili ya makundi na kuondolewa katika michuano hiyo.
Ikiwa Adel Amrouche raia wa Algeria atapewa kibarua hicho, atakuwa amevuka mpaka kutoka jijini Nairobi kuja Dar es salaam, baada ya kuiongoza Harambee Stars kunyakua taji la CECAFA mwaka 2013.
Uzoefu wake kuhusu soka barani Afrika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cogo Burundi, Equitorial Guinea na Kenya huenda kukaivutia Tanzania.