Timu ya taifa ya soka ya Namibia imefuzu katika hatua ya robo fainali katika michuano ya kutafuta taji la COSAFA baina ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika.
Namibia ilifuzu katika hatua hiyo kutoka kundi la A baada ya kumaliza kundi hilo kwa wingi wa alama saba na kupata ushindi muhimu Alhamisi usiku baada ya kuishinda Zimbabwe mabao 4 kwa 1.
Katika mchuano mwingine, Mauritius nao waliwashinda Ushelisheli bao 1 kwa 0.
Namibia sasa itamenyana na Zambia katika hatu hiyo ya robo fainali juma lijalo.
Leo ni michuano ya kumaliza kundi la B, na mchuano muhimu leo ni katia ya Madagascar na Swaziland kwa sababu ni timu moja tu ndio itakayofuzu katika hatua hiyo.
Madagascar na Swaziland zote zina alama 6.
Atakayefuzu atacheza na Ghana katika hatua ya nusu fainali.
Mchuano mwingine ni kati ya Tanzania na Lesotho zote ambazo zimeondolewa katika michuano hiyo kwa matokeo mabaya.
Tanzania ambayo imepata ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashabiki wa soka nyumbani inalenga kupata ushindi leo usiku ili kurudi nyumbani na angalau kitu mkononi kutuliza hasira za mashabiki.