Na Victor Abuso, Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Florent Ibengé Ikwange amekitaja kikosi cha wachezaji 25 kuanza maandalizi ya michuano ya kufuzu kucheza michuano ya Afrika AFCON mwaka 2017 nchini Gabon. DRC ambayo inafahamika kwa jina maarufu kama Leopards imejumuishwa katika kundi moja na majirani zao Angola, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Madagascar. Leopards itaanza mchuano wake wa ufunguzi jijini Kinshasa dhidi ya Madagascar tarehe 14 mwezi ujao. Kabla ya michuano hiyo, DRC itamenyana na Burkina Faso tarehe 3 mwezi ujao kabla ya kupambana na Cameroon tarehe 9 katika michuano ya kimataifa ya kirafiki. Hii ndio orodha ya wachezaji waliotajwa na kocha Florent Ibengé Ikwange: KIASSUMBUA JOEL (FC WOHLEN - Switzerland) KUDIMBANA NICAISE (Anderlecht Belgium) MANDANDA PERFECT (CHARLEROI, Belgium) ISSAMA MPEKO OJ (KABUSSCHORP - Angola) OUALEMBO CHRISTOPHER (ACADEMICA Coimbra - Portugal) Mongongu CEDRIC (Evian Thonon Gaillard -France) GABRIEL Zakuani (PETERBOROUGH - Great Britain) KIMWAKI Mpela JOEL (TP MAZEMBE - RD Congo) MAVINGA CHRIS (STADE DE REIMS - France) N'SAKALA FABRICE (Anderlecht Belgium) TAMATA ABEL (PSV EINDOVHEN - Netherlands) KAMAVUAKA Wilson (STURM GRAZ - Austria) Youssuf Mulumbu (WBA - Great Britain) MAGHOMA JACQUES (SHEFFIELD WEDNESDAY - Great Britain) NZUZI TOKO (Eskisehirspor - Turkey) Kebano Neeskens (Charleroi-Belgium) MBEMBA CHANCEL (Anderlecht Belgium) BOTAKA JORDAN (EXCELSIOR ROTTERDAM -Country Netherlands) LUKOKI JODY (PEC SWOLLE-Netherlands) MABWATI CEDRIC (OSSASUNA Pamplona-Spain) BEZUA Dieumerci Mbokani (Dynamo Kiev-Ukraine) Bokila JEREMY (TEREK GROZNY - Russian) BOLASIE YALA YANNICK (CRYSTAL PALACE - Great Britain) Ndongala dieumerci (Charleroi-Belgium) Bakambu CEDRIC (BURSASPOR - Turkey)
DRC: Florent Ibenge ateua kikosi kuanza maandalizi ya kufuzu AFCON 2017
DRC: Florent Ibenge ateua kikosi kuanza maandalizi ya kufuzu AFCON 2017
More in
-
Nigeria Super Falcons break jinx and qualify for Paris 2024 Olympics
Nigeria Super Falcons have qualified for the 2024 Paris Olympic Games. Nigeria beat South...
-
Zambia Copper Queens qualify for 2024 Paris Olympics
The Zambia Women’s National Team, The Copper Queens have booked a place at the...
-
Cameroon sports Minister appoints Indomiable lions coach in Bizzare move
Cameroon Sports minister Narcisse Mouelle Kombi has appointed Belgian Marc Brys as the new...
-
Simba lose to Al Ahly at home in first leg Quarter-final
Tanzanian giants Simba SC suffered a devastating 1-0 defeat to record holders Al Ahly...