Na Victor Abuso, Wachezaji wawili wa klabu ya soka ya TP Mazembe nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiongozwa na mlinda mlango Robert Muteba Kidiaba, wamewasilisha maombi ya kuwania ubunge katika jimbo la Katanga. Pamoja na Kidiaba ambaye anafahamika sana kwa mtindo wa kusherehekea bao kwa kuruka kwa makalio. Pamphile Mihayo Kazembe pia ni mchezaji mwingine wa TP Mazembe anayewania ubunge kupitia chama cha upinzani cha PND. Nahodha huyo wa Leopards mwenye umri wa miaka 39 amesema anaamini kuwa wachezaji wanaweza kuwa viongozi bora na kuleta mabadiliko ya maendeleo katika maeneo yao. Uchaguzi wa wabunge na urais utafanyika mwaka ujao nchini humo na ikiwa Kidiaba atachaguliwa kuwa mbunge, bila shaka itakuwa ni historia katika mchezo wa soka nchini humo. Kidiaba alianza kuichezea timu ya taifa mwaka 2002 na ameshiriki katika michuano 11 ya kufuzu katika michuano ya kombe la duniani na kwa ujumla kuichezea timu ya taifa mara 59. Mwezi Desemba, mwaka 2014 alitangaza kuwa alikuwa anajiuzulu baada ya michuano ya mwaka huu ya mataifa bingwa barani Afrika lakini baadaye akabadilisha mawazo ya kuendelea kucheza soka.
DRC:Kipa mwenye “madoido” Robert Kidiaba kuwania ubunge
DRC:Kipa mwenye “madoido” Robert Kidiaba kuwania ubunge
More in
-
Vinícius Júnior Honored with Certificate Celebrating His African Heritage
Photo by Heuler Andrey/Eurasia Sport Images/Getty Images In a heartfelt moment before Brazil’s...
-
Zimbabwe Afcon hopes dashed after loss to Cameroon
Zimbabwe’s hopes of finishing the 2025 Africa Cup of Nations (AFCON) qualifiers undefeated were...
-
Zambia end Afcon campaign with comfortable win over Sierra Leone
Zambia ended their 2025 Africa Cup of Nations qualifying campaign on a high after...
-
Tanzania,Mozambique,Botswana Qualify for Afcon 2025 in Morocco
Tanzania, Botswana and Mozambique have secured the final berths at the 2025 Africa Cup...