Connect with us

Shirikisho la soka nchini Afrika Kusini SAFA, limemteua Stuart Baxter kuwa kocha mpya wa timu ya taifa Bafana Bafana.

 Raia huyu wa Uingereza mwenye umri wa miaka 63, anarejea kuifunza Afrika Kusini baada ya kufanya hivyo mara ya kwanza kati ya mwaka 2004-2005.

Kocha huyu wa zamani wa klabu ya Kaizer Chiefs na SuperSport United zote za Afrika Kusini, anachukua nafasi ya Shakes Mashaba ambaye alifutwa kazi mwishoni mwa mwezi mwaka uliopita kwa sababu ya matokeo mabaya.

Msemaji wa Shirikisho hilo Dominic Chimhavi amesema mambo yote yameshakamilika, na atakabidhiwa rasmi timu ya taifa siku ya Ijumaa.

Ripoti zinasema kuwa atalipwa mshahara wa Rand Milioni 12 kwa mwaka.

Baxter ambaye alianza kufunza soka mwaka 1985. Amewahi kuifunza timu ya vijana ya Uingereza wenye chini ya umri wa miaka 19 kati ya mwaka 2002 na 2004.

Kati ya mwaka 2008 na 2010 aliwahi kuifunza timu ya taifa ya Finland.

Kazi kubwa ya Baxter itakuwa ni kuisaidia Afrika Kuisni kufuzu katika fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi lakini pia michuano ya CHAN nchini Kenya mwakani.

More in