Klabu ya soka ya CS Sfaxien kutoka Tunisia, imekuwa klabu ya kwanza kufuzu katika hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho barani Afrika.
CS Sfaxien ilifika katika hatua hiyo baada ya kuishinda Rail club du Kadiogo ya Burkina Faso kwa mabao 4-1 baada ya mchuano wa mzunguko wa pili siku ya Ijumaa.
Mchuano wa kwanza CS Sfaxien ilishinda mabao 2-1 na kupata ushindi mwingine wa mabao 2-0 walipocheza nyumbani.
Mabao kutoka kwa Maher Hannachi na Karim Aouadhi yalitosha kuifikisha CS Sfaxien katika hatua hiyo.
Mabingwa watetezi TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Jumapili itakuwa ugenini kumenyana na JS Kabylie ya Algeria.
Mechi ya kwanza mjini Lubumbashi, Mazembe walipata ushindi wa mabao 2-0.
Mechi za Jumamosi Aprili 15 2017:-
MC Alger (Algeria) vs Young Africans (Tanzania). Mechi ya kwanza Yanga ilishinda 1-0.
Mbabane Swallows (Swaziland) vs AC Leopard (Congo). Mechi ya kwanza, AC Leopard ilishinda bao 1-0.
MAS Fez(Morocco) vs FUS Rabat ( Morocco). Mechi ya kwanza FUS Rabat ilishinda mabao 2-1.
ZESCO United (Zambia) vs Enugu Rangers (Nigeria). Mechi ya kwanza, timu zote mbili zilitoka sare ya mabao 2-2.
Al Masry ( Misri) vs KCCA (Uganda). Mechi ya kwanza, KCCA ilishinda bao 1-0.
Recreativo do Libolo ( Angola) vs CnaPS Sport( Madagascar). Mechi ya kwanza timu zote zilitoka sare ya bao 1-1.
Mechi za Jumapili Aprili 16 2017:-
AS Tanda (Ivory Coast) vs Platinum Stars ( Afrika Kusini).
Barrack Young Controllers (Liberia) vs Supersport United (Afrika Kusini).
ASEC Mimosas (Ivory Coast ) vs CF Mounana ( Gabon).
Rivers United ( Nigeria) vs Rayon Sport (Rwanda)