Connect with us

Klabu ya wanawake ya Lushoises OCL City mabingwa nchini DRC

Klabu ya wanawake ya Lushoises OCL City mabingwa nchini DRC

Na Victor Abuso,

Lushoises OCL City  ndio mabingwa wa soka taji la wanawake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuwashinda Recoilless ya Mbuji-Mayi mabao 3 kwa 0 katika mechi ya fainali.

Hili ni taji la nne mfululizo  kwa klabu ya  Lushoises, iliyoanza kushiriki soka la wanawake nchini humo  tangu mwaka 2012.

Mwaka uliopita, vlabu hivi vilikutana tena katika hatua ya fainali na akina dada kutoka Lubumbashi wakaendelea kudhihirisha kuwa wao ni moto wa kuotea mbali.

Nafasi ya tatu ilinyakuliwa na Bafana Bafana Katanga baada ya kuwafunga Mornng Star kutoka North Kivu mabao 6 kwa 1.

Mikoa 9 kati ya 11 ilishiriki  katika makala haya ya nane ya michuano hii huku mikoa ya Kasai  Occidental na  Ecuador ikijiondoa kwa sababu za changamoto za kifedha.

Orodha ya vlabu vilivyoshiriki katika ligi hiyo:-

Bilenge (Kinshasa)
Bafana Bafana (Katanga)
RC Boa (Maniema)
Promo Sport (Bas-Congo)
GTT (Bandundu)
Attack recoilless (Kasai Oriental)
Morning Star (South Kivu)
OCL into City (Katanga)

Orodha ya mabingwa wa taji hilo

2008 South Kivu
2009 Kinshasa
2010 Kinshasa
2011 Katanga
2012 OCL City
2013 OCL City
2014 OCL City
2015 OCL City.

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in