Na Victor Abuso,
Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars Bobby Williamson amewaacha wachezaji wa klabu ya AFC Leopards baada ya uongozi wa klabu hiyo kuamuru kuwa warudi kambini kuendelea na maandalizi ya kuwania taji la ligi kuu.
Harambee Stars imekuwa ikijiandaa katika michuano ya kufuzu kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon na hatua hii ya uongozi wa AFC inaamanisha kuwa wachezaji hao watakosa kuliwakilisha taifa.
Kenya itaanza safari ya kusaka tiketi hiyo dhidi ya Congo Brazaville Jumamosi ijayo ugenini.
Kikosi cha Williamson kinaelekea jijini Kigali nchini Rwanda siku ya Ijumaa kuanza kambi na pia kushiriki katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Tanzania siku ya Jumamosi.
Wachezaji wa Gor Mahia wataungana na wachezaji wengine baada ya mchuano wao wa ligi kuu dhidi ya Tusker mjini Kisumu.
Nahodha wa Stars ni Victor Wanyama anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Southamptom nchini Uingereza , anaongoza kikosi cha wachezaji wakulipwa kuiwakilisha Kenya katika mchuano huo wa kimataifa.
Mbali na Congo Brazavile, Kenya imejumuishwa pamoja na Zambia na Guine Bissau.
Kikosi kamili
Makipa:
Goalkeepers: Joseph Baraza and Ian Otieno(Rangers)
Mabeki: Charles Odette(Sony Sugar) , Evans Maliachi(Muhoroni Sugar), David Ochieng(Al Tawoon), Brian Mandela(Santos)
Viungo wa Kati: Antony Akumu(Al Khartoum), Stephen Wakanya(Chemelil), Peter Nzuki(Nakumatt), Victor Wanyama(Southampton)
Washambulizi: Allan Wanga(Al M ereikh), Francis Kahata(FK Tirana).
Wachezaji wa Gor Mahia watakaojiunga na wenzao jijini Kigali ni pamoja na, Musa Mohammed, Harun Shakava,Victor Ali Abondo,Bonface Oluoch,Collins Okoth,Michael Olunga na kipan wa makipa Mathew Ottamax.