Connect with us

Rais wa Shirikisho la soka nchini Ghana Kwesi Nyantankyi ameteuliwa kuwa naibu rais wa kwanza wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Hatua hiyo ilifanyika katika mkutano Mkuu wa dharura wa CAF, pembezoni mwa mkutano wa FIFA uliofanyika siku ya Jumatatu mjini Manama nchini Bahrain.

Naye rais wa Shirikisho la soka nchini DRC Constant Omari ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa CAF,Issah Hayatou, aliteuliwa kuwa makamu wa pili wa rais wa CAF.

Wawili hawa watamsaidia rais wa CAF Ahmed Ahmed ambaye amenukuliwa akisema hatapokea mshahra wowote kwa kipindi cha miaka minne atakachokuwa kiongozi wa Shirikisho hilo.

Rais wa Shirikisho la soka nchini Uganda Mhandisi Moses Magogo ameteuliwa kuketi katika Kamati kuu ya CAF.

Kamati ya kuangazia soka la wanawake itaongozwa na rais wa Shirikisho la soka nchini Sirrra Leon Isha Johansen .

Amaju Pinnick rais wa Shirikisho la soka nchini Nigeria ataongoza Kamati ya michuano ya mataifa bingwa barani Afrika na maswala ya wanahabari.

Rais wa Shirikisho la soka nchini Afrika Kusini Danny Jordaan ataongoza Kamati ya maswala ya masoko na matangazo.

 

More in