Na Victor Abuso, Vyombo vya Habari nchini Uingereza zinaripoti kuwa, Morocco ndio iliyoshinda kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 wala sio Afrika Kusini. Hizi ni tuhma za hivi punde za kashfa za ufisadi zinazoendelea kulikabili Shirikisho la soka duniani FIFA. Ripoti zinasema kuwa Morocco iliishinda Afrika Kusini kwa zaidi ya kura mbili kwa mujibu wa siri iliyotolewa na aliyekuwa Mwanakamati Mkuu wa FIFA Ismail Bhamjee. Juma lililopita, Marekani ilidai kuwa uchunguzi wa wajajusi wa FBI umebaini kuwa Serikali ya Afrika Kusini ilitoa Dola Milioni 10 kupitia aliyekuwa Naibu rais wa FIFA Jack Warner ili kupigiwa kura na kuwa wenyeji wa kobe la dunia. Hata hivyo, Waziri wa Michezo wa Afrika Kusini Fikile Mbalula alijitokeza na kukanusha madai hayo na kusema fedha hizo zilitolewa kwa lengo la kuendeleza na kusaidia soka katika mataifa ya Carrebian. Bhamjee ananukuliwa akisema baada ya kuhojiwa na mwahabari mmoja kuwa, licha ya Morocco kushinda nayo pia ilitoa rushwa ya Dola Milioni 1 kwa kiogozi wa CONCACAF Jack Warner ili kupigiwa kura. Sakata hili la FIFA limesababisha Joseph Blatter kutangaza kuwa anajiuzulu na anatarajiwa kuitisha mkutano mkuu ili kufanyika kwa uchaguzi mwingine, mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka ujao. Jack Warner aliyeondoka katika uongozi wa FIFA miaka minne iliyopita, juma lililopita alidokeza kuwa atatoa siri ambazo amekuwa akizihifadhi kuhusu kashfa ya ufisadi katika Shirikisho hilo la soka duniani. Sakata hili la rushwa pia limesababisha kuwepo kwa dukuduku kuhusu usafi wa Urusi kupewa nafasi ya wenyeji wa kombe la duniani mwaka 2018 pamoja na Qatar mwaka 2022.
Ripoti: Morroco ilishinda wenyeji wa kombe la dunia 2010
Ripoti: Morroco ilishinda wenyeji wa kombe la dunia 2010
More in
-
Vinícius Júnior Honored with Certificate Celebrating His African Heritage
Photo by Heuler Andrey/Eurasia Sport Images/Getty Images In a heartfelt moment before Brazil’s...
-
Zimbabwe Afcon hopes dashed after loss to Cameroon
Zimbabwe’s hopes of finishing the 2025 Africa Cup of Nations (AFCON) qualifiers undefeated were...
-
Zambia end Afcon campaign with comfortable win over Sierra Leone
Zambia ended their 2025 Africa Cup of Nations qualifying campaign on a high after...
-
Tanzania,Mozambique,Botswana Qualify for Afcon 2025 in Morocco
Tanzania, Botswana and Mozambique have secured the final berths at the 2025 Africa Cup...