Timu ya taifa ya soka ya Zambia yenye wachezaji chini ya miaka 20, imefuzu katika hatua ya robo fainali kuwania kombe la dunia katika michuano inayoendelea nchino Korea Kusini.
Mabingwa hao wa Afrika walitoka nyuma na kuifunga Ujerumani mabao 4-3 katika muda wa nyongeza, baada ya timu zote kutofungana katika muda wa kawaida.
Zambia ilionekana kuwa imeshinda mechi hiyo baada ya kuongoza kwa mabao 3-1 katika dakika ya 89, lakini wachezaji wa Ujerumani Suat Serdar na Jonas Arweiler walifunga mabao ya haraka na kufanya mambo kuwa sare ya mabao 3-3.
Hata hivyo, Shemmy Mayembe alikuwa shujaa wa Zambia, baada ya kufunga bao la nne na la ushindi na mchuano huo kumalizika kwa ushindi wa mabao 4-3. Wafungaji wengine wa Zambia ni pamoja na Emmanuel Banda, Enock Mwepu na Fashion Sakala.
Zambia sasa watachuana na Ufaransa au Italia katika hatua ya robo fainali.
Wawakilishi wengine wa Afrika Senegal, watamenyana na Mexico siku ya Alhamisi.
Mbali na Zambia, Uingreza, Uruaguay, Ureno na Venezuela zimefuzu katika hatua ya robo fainali.