Connect with us

Klabu ya soka ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya, imewasili jijini Dar es salaam nchini Tanzania tayari kumenyana na klabu ya Everton ya Uingereza katika mchuano wa Kimaifa wa kirafiki.

Mchuano huo utachezwa katika uwanja wa Taifa siku ya Alhamisi.

Mechi hiyo ya kirafiki imeandaliwa na kampuni ya michezo ya kubahatisha, ya Sportpesa.

Gor Mahia ndio mabingwa wa taji makala ya kwanza ya Sportpesa kati ya vlabu vya soka kutoka nchini Kenya na Uganda.

Mchuano huo wa kirafiki utakuwa wa kwanza kwa kocha mpya Dylan Kerr. Kampuni ya Sportpesa inafadhili vlabu hivyo viwili.

Mgombea urais kupitia muungano wa upinzani NASA, Raila Odinga ambaye ni mlezi wa Gor Mahia anatarajiwa kuhudhuria mchuano huo wa kirafiki.

More in