Connect with us

Hatua ya robo fainali kuwania ubingwa wa taji la Klabu bingwa na Shirikisho katika mchezo wa soka, inachezwa mwishoni mwa wiki hii katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Vlabu nane, vinashiriki katika hatua hii muhimu kutafuta taji la klabu bingwa na Shirikisho.

Michuano hii inachezwa nyumbani na ugenini na washindi watafuzu katika hatua ya nusu fainali.

Supersport United ya Afrika Kusini inafungua dimba ya hatua hii kuwania taji la Shirikisho dhidi ya ZESCO United ya Zambia siku ya Ijumaa usiku.

Siku ya Jumamosi, MC Alger itakuwa nyumbani jijini Algers kupambana na Club Africain ya Tunisia, huku FUS Rabat ya Morocco ikikabiliana na CS Sfaxien ya Tunisia.

Wawakilishi wa Sudan Al-Hilal Al-Ubayyid nao watawakaribisha TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Michuano ya marudiano itachezwa baada ya wiki moja.

Kuhusu michuano ya klabu bingwa barani Afrika, siku ya Jumamosi, Al-Ahly itapambana na Esperance de Tunis ya Tunisia, huku Ferroviario Beira ya Msumbuji ikimenyana nyumbani na USM Alger.

Siku ya Jumapili, kutakuwa na michuano miwili. Al-Ahly Tripoli ya Libya itachuana na Etoile du Sahel ya Tunisia huku mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wakiwa nyumbani kumenyana na Wydad Casablanca ya Morocco.

Nusu fainali ya kwanza inatarajiwa kuchezwa mwisho wa mwezi Septemba huku fainali ikiuchezwa uyumbani na ugenini.

More in