Na Victor Abuso
Mataifa saba ya Afrika yatakayoshiriki katika michuano ya soka kuwania ubingwa wa Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 23 itakayofanyika kati ya tarehe 28 mwezi Novemba hadi tarehe 12 mwezi Desemba nchini Senegal yameshafahamika rasmi
Mataifa hayo ni pamoja na wenyeji Senegal, Algeria, Misri, Zambia, Tunisia, Afrika Kusini, Nigeria na Mali.
Zambia, Tunisia na Mali zimefuzu katika michuano hii kwa mara ya kwanza.
Michuano ya mwisho ya kufuzu ilichezwa mwishoni mwa juma lililopita na washindi kupatikana.
Nigeria ilifuzu baada ya kuifunga Congo Brazaville mabao 2 kwa 1.
Algeria iliishinda Sierra Leone mabao 2 kwa 0, huku Mali ikiilaza Gabon mabao kwa 0.
Vijana wa Misri, waliwachabanga Uganda mabao 6 kwa 1, baada ya kushindwa mabao 4 kwa 0 jijini Cairo na nyumbani kulemewa kwa mabao 2 kwa 1.
Afrika Kusini nayo iliishinda Zimbabwe kwa jumla ya mabao 4 kwa 1, huku Tunisia wakiwalemea Morocco mabao 2 kwa 1.
Zambia baada ya kutoka sare ya kutofungana na Ivory Coast nyumbani na ugenini ilifuzu baada ya kupata ushindi wa penalti 4 kwa 3.
Michuano hiyo pia itatumiwa kutafuta timu tatu za kwanza kufuzu katika michezo ya msimu joto ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mwaka ujao.
CAF: Mataifa yatakayoshiriki fainali za Vijana yafahamika
CAF: Mataifa yatakayoshiriki fainali za Vijana yafahamika
More in
-
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
TP Mazembe have won the 2024 CAF Women’s Champions League title after they defeated...
-
Vinícius Júnior Honored with Certificate Celebrating His African Heritage
Photo by Heuler Andrey/Eurasia Sport Images/Getty Images In a heartfelt moment before Brazil’s...
-
Zimbabwe Afcon hopes dashed after loss to Cameroon
Zimbabwe’s hopes of finishing the 2025 Africa Cup of Nations (AFCON) qualifiers undefeated were...
-
Zambia end Afcon campaign with comfortable win over Sierra Leone
Zambia ended their 2025 Africa Cup of Nations qualifying campaign on a high after...