Mshambuliaji wa klabu ya soka ya Gor Mahia nchini Kenya Meddie Kagere ndio mchezaji bora nchini humo kwa mwaka 2017.
Mchezaji huyo kutoka nchini Rwanda, aliisaidia klabu yake ya Gor Mahia kunyakua taji la ligi kuu kwa mara 16 kwa kufunga mabao 14 na kusaidia kufungwa kwa mabao 18.
Mwaka 2015, aliibuka katika nafasi ya pili mbele ya Michael Olunga ambaye siku hizi anacheza soka la kulipwa katika klabu ya Girona nchini Uhispania.
Mwaka 2016, mshindi alikuwa ni Kenneth Muguna ambaye pia ni mshambuliaji wa Gor Mahia.
Historia fupi ya Kagere:-
Kabla ya kusajiliwa na klabu ya Gor Mahia, aliwahi kuichezea KF Tirana ya Albania, Rayon Sport, Police FC, Kiyovu Sports na Atraco FC zote za Rwanda.
Kagere mwenye umri wa miaka 31, pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Amavubi Stars.
Orodha kamili ya washindi:-
- Mchezaji bora
- Meddie Kagere
Kipa bora
- John Oyemba – Kariobangi Sharks
- David Juma- Kakamega Homeboyz
- Patrick Matasi – Posta Rangers
Beki bora
- Musa Mohammed – Gor Mahia
- Jockins Atudo- Posta Rangers
- Godfrey Walusimbi – Gor Mahia
Kiungo wa Kati
- George ‘Blackberry’ Odhiambo – Gor Mahia
- Lawrence Juma- Nzoia Sugar FC
- Michael Madoya – Zoo FC
Mchezaji Chipukizi
- Nicholas Kipkirui –Zoo FC
- Vincent Oburu –AFC Leopards
- Brian Otieno – Nzoia Sugar FC
Mfungaji bora
- Masoud Juma – Kariobangi Sharks
- Meddie Kagere – Gor Mahia
- Kepha Aswani – Nakumatt FC
- Jacques Tuyisenge – Gor Mahia
- Stephen Waruru- Ulinzi Stars