Connect with us

Azam imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya na kupanda hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Azam imefikisha alama 30 na kuisshusha Simba hadi nafasi ya pili ikiwa na alama 29. Simba inatarajiwa kucheza kesho na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba, Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Bao la kwanza la Azam lilipatikana katika dakika ya 70 kupitia beki wake, Yakubu Mohamed.
Wakati Prisons wakipambana kusawazisha, Paul Peter aliandika bao la pili katika dakika ya 81 na kuihakikishia Azam FC pointi tatu.

Yanga baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Mwadui wiki iliyopia leo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting bao lililofungwa na kiungo Pius Buswita.

Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha alama 25 na kupanda hadi nafasi ya hadi kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in