Connect with us

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Misri, na mchezaji wa klabu ya Liverpool Mohamed Salah amesema ana amini kuwa atakuwa amepata nafuu kabla ya kuanza kwa fainali ya kombe la dunia tarehe 24 mwezi Juni nchini Urusi.

Salah alipata jeraha la bega mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati klabu yake ilipokuwa inamenyana na Real Madrid katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.

Upendo wenu na uugwaji mkono, utanipa nguvu,” amesema Salah.

Misri itaanza kampeni yake ya kutafuta ubingwa wa kombe la dunia dhidi ya Uruguay.

Salah, anatarajiwa kuisaidia timu yake ya taifa wakati huu akiwa na rekodi ya kuifungia klabu yake mabao 44 msimu uliopita.

More in