Na Victor Abuso, Wapinzani Nigeria na Cameroon wametenganishwa katika michuano ya hatua ya makundi kuwania kombe la Afrika kwa vijana wasiozidi miaka 17 itakayochezwa mwaka 2019 nchini Tanzania. Droo hiyo ilifanyika Alhamisi usiku jijini Dar es salaam, kuelekea michuano hiyo itakayochezwa mwezi Aprili. Timu nyingine iliyopangwa katika kundi hilo ni pamoja na wenyeji Tanzania na jirani zao Uganda, ambao watacheza katika michuano hii kwa mara ya kwanza pamoja na Angola. Cameroon ambao walishinda taji hili mwaka 2003, wamepangwa katika kundi moja na Guinea, Morocco na Senegal. Michuano hiyo itatumiwa pia kutafuta nchi tatu, zitakazoliwakilisha bara la Afrika katika fainali za kombe la dunia nchini Peru mwaka ujao. Kundi A – Tanzania, Nigeria, Angola, Uganda Kundi B – Cameroon, Guinea, Morocco, Senegal. |
Related Topics



CAF Confederation Cup
Simba book final spot in CAF Confederation cup

CAF Confederation Cup
Simba book final spot in CAF Confederation cup
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 5 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...