-
by
Victor Abuso
Kipa wa muda mrefu wa timu ya taifa ya soka ya Nigeria Vincent Enyeama ametangaza kuacha kuichezea timu yake ya taifa.
Hatua hii inakuja baada ya kufanya mashauriano na viongozi wakuu wa Shirikisho la soka nchini Nigeria NFF nchini Ubelgiji.
Hatua hii haijawashangaza wapenzi wa soka nchini Nigeria kwa sababu hivi karibuni alionekana kutofautiana na kocha Sunday Oliseh baada ya kumteua mshambuliaji wa CSKA Moscow Ahmed Musa.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 33 anayecheza soka la kulipwa nchini Ufaransa katika klabu ya Lille mwaka uliopita baada ya kustaafu kwa beki Joseph Yobo alinukuliwa akisema muda wake wa kuachana na Nigeria ulikuwa haujafika.
Enyeama ametangaza uamuzi wake kupitia ukurasa wake Instagram.
“Nimepigana vita vizuri kwa miaka 13.Nimemaliza kazi yangu.Nimelinda amani na kuimba wimbo wa taifa kwa hisia,” aliandika.
“Mungu ibariki Nigeria.Kuanzia siku zijazo mimi sio nahodha wa Nigeria tena.Mimi sio kipa wa timu ya taifa, nimeachana na timu ya taifa,”.
Mwezi Juni, Nigeria ikicheza na Chad Enyeama aliichezea timu yake mchuano wake wa 101 na kuweka historia kwa kuichezea nchi yake kwa muda mrefu.
Kipa huyo atakumbukwa kuichezea Nigeria katika Makala matatu ya kombe la dunia na kuingoza nchi yake kushinda taji la Afrika mwaka 2013.
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
CAF Champions League
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns Off to a Lukewarm Start in 2024/25 CAF Champions League
CAF Champions League
AL Ahly start CAF CL campaign with win over Stade d’Abidjan
CAF Confederation Cup
Simba make good start beating Bravos do Maquis
CAF Confederation Cup
Enyimba fall to Al Masry in Alexandria
CAF Confederation Cup
Zamalek got their Group D campaign off to a comfortable star
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...