-
by
Victor Abuso
Shirikisho la soka duniania FIFA limeidhinisha majina ya watu watano kati ya saba walioomba nafasi ya kuwania urais wa Shirikisho hilo wakati uchaguzi mpya utakapofanyika mwezi Februari mwaka ujao.
Wagombea walioidhinishwa ni pamoja na Mwanamfalme wa Jordan Ali Al Hussein, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa, Jerome Champagne, Gianni Infantino na Tokyo Sexwale raia wa Afrika Kusini.
Kamati ya nidhamu na maadili inasema hatima ya Mitchel Platini rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya aliyesimamishwa kwa siku tisini kutojihusisha na maswala ya soka kwa tuhma za ufisadi, itafahamika baada ya muda huo kukamilika.
Rais wa Shirikisho la soka nchini Liberia Musa Bility, ndio mgombea pekee ambaye hadi sasa ameondolewa kabisa katika kinyang’anyiro hicho.
Kamati hiyo ya FIFA inasema imemwondoa Bility katika orodha hiyo kwa sababu ya kuwa na rekodi mbaya ya nidhamu.
Platini ambaye amekuwa akipewa nafasi kubwa ya kushinda taji hilo, huenda akapewa nafasi ya kugombea ikiwa atapatikana bila kosa kuhusu tuhma za kupokea Dola Milioni 2 kutoka kwa rais wa FIFA Sepp Blatter mwaka 2011.
Mawakili wa Platini wanasema wanasikitishwa mno na FIFA kwa namna inavyochukua muda mrefu kuamua hatima yake.
Mitchel Platini ameendelea kusisitiza kuwa hana kosa lolote.
CAF Confederation Cup
Simba snatch late winner against CS Sfaxien as Enyimba beaten
CAF Champions League
Sundown CL campaign has a pulse after beating Raja
CAF Champions League
TP Mazembe win CAF Women’s Champions league trophy
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns Off to a Lukewarm Start in 2024/25 CAF Champions League
CAF Champions League
AL Ahly start CAF CL campaign with win over Stade d’Abidjan
CAF Confederation Cup
Simba make good start beating Bravos do Maquis
CAF Confederation Cup
Enyimba fall to Al Masry in Alexandria
CAF Confederation Cup
Zamalek got their Group D campaign off to a comfortable star
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...