-
by
Victor Abuso
Hatua ya nusu fainali kuwania ubingwa wa mwaka 2015 katika mchezo wa soka baina ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA inachezwa leo Alhamisi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Mchuano wa kwanza unawakutanisha mabingwa wa mwaka 2006 Sudan dhidi ya Amavubi Stars ya Rwanda.
Mwaka 2006 wakati michuano hii ilipoandaliwa tena nchini Ethiopia, Sudan walifika katika hatua ya nusu fainali na baadaye kufuzu hadi fainali na kuwashinda wageni Zambia kupitia mikwaju ya penalti.
Licha ya kufungwa na Malawi mabao 2 kwa 1 na kutoka sare ya kutofungana na jirani yake Sudan Kusini, Falcon FC wamejikakamua na kufika katika hatua ya nusu fainali.
Mara ya mwisho Sudan kufika katika hatua ya fainali katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 2013 wakati mashindano haya yalipofanyika jijini Nairobi nchini Kenya na wenyeji Harambee Stars kuibuka mabingwa.
Rwanda nayo mara ya mwisho kufika fainali ilikuwa ni mwaka 2009.
Kocha wa Amavubi Stars John McKinstry ameweka matumaini yake kwa wachezaji kama Jacques Tuyisenge na Haruna Niyonzima ambao wameonekana kuchangia mafanikio kwa timu yao.
Ethiopia vs Uganda
Huu ni mchuano utakaowavutia mashabiki wengi kwa sababu Ethiopia wako nyumbani.
Uganda pia inaangaziwa kwa karibu na kila mmoja kutokana na rekodi yake nzuri ya kunyakua mataji 13 ya CECAFA.
Cranes wanaofunzwa na kocha Milutin Micho Sredojevic wanalenga kuwashinda wenyeji na kufika fainali kulisaka taji la 14 kurudi nalo jijini Kampala.
Uganda walianza vibaya baada ya kufungwa na watani wao wa jadi Kenya mabao 2 kwa 0 lakini wakaedelea kuandkisha matokeo mazuri, dhidi ya Zanzibar na Burundi katika kundi lao.
Mara ya mwisho mataifa haya kukutana ilikuwa ni mwezi Novemba mwaka jana , mchuano ambao Uganda waliibuka washidi kwa kupata mabao 3 kwa 0 jijini Kampala.
Hadi kufika katika hatua ya nusu fainali, Ethiopia kwa jina maarufu kama Walia Ibex walianza vibaya kwa kufungwa na Rwanda bao 1 kwa 0 lakini baadaye wakashinda Somalia mabao 2 kwa 0 na kufuzu baada ya sare ya bao 1 kwa 1 na Tanzania bara na baadaye kukutana tena na Kilimanjaro Stars katika hatua ya robo fainali na kuwashinda kupitia mikwaju ya penalti.
Kocha wa Yohannes Sahle amewaambia wachezaji wake kucheza kwa nguvu dakika zote 90 na kutafuta mabao ya mapema dhidi ya Uganda timu ambayo anakiri ni nzuri.
Uganda Cranes na Ethiopia Walia ibex wamekutana mara 35 katika michuano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo 10 ya CECAFA.
Uganda wameshinda mara 14 na Ethiopia mara 13 na kutoka sare mara nane.
Washindi katika nusu fainali zote watamenyana katika mchuano wa fainali siku ya Jumamosi jijini Addis .
CAF Champions League
Mamelodi Sundowns and Asfar advance to Quarter-finals
CAF Champions League
TP Mazembe bow out with big win over leaders Al Hilal
CAF Champions League
MC Alger book Quarter-finals spot after draw with Yanga
CAF Champions League
Orlando Pirates capped their incredible with Al Ahly win
Women's Football
FAZ appoints Hauptle as new Copper Queens Coach
Africa Cup of Nations
CAF Slaps Libya with $50,000 fine, Benin also sanctioned
CAF Champions League
Raja Casablanca upset Mamelodi Sundowns
CAF Champions League
Mouth Watering CAF Champions League matches lined up
CAF Champions League
Al Ahly, Al Hilal Omdurman and Esperance looking to book Quarter-finals slot
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...