Klabu ya AFC Leoapards ya Kenya na Yanga FC ya Tanzania zimefuzu katika hatua ya robo fainali kuwania taji la Sportpesa Super Cup.
Leopards ilikuwa ya kwanza kufuzu baada ya kuifunga Singida United ya Tanzania kwa mabao 5-4 baada ya mikwaju ya penalti.
Kabla ya hatua hiyo, timu zote mbili zilitoka sare ya bao 1-1 katika muda wa dakika 90 uliokuwa umepangwa kumtamfuta mshindi.
Hali ilikuwa vivyo hivyo kwa mabingwa wa Kenya Tusker FC, iliyopoteza dhidi ya mabingwa wa Tanzania bara Yanga FC, kwa kufungwa mabao 5-3 kupitia mikwaju ya penalti, Jumatatu jioni katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Timu zote mbili zilionesha mchezo wa hali ya juu, huku zikijaribu mashambulizi ambayo hayakuzaa matunda.
AFC Leopards sasa itamenyana na Yanga katika hatua ya nusu fainali ya michuano hii.
Jumanne Juni 6 2017
-
Gor Mahia (Kenya) vs Jang’ombe Boys FC (Zanzibar)
-
Simba SC (Tanzania) vs Nakuru All Stars (Kenya)
Tuzo
-
Mshindi -Dola za Marekani 30,000
-
Mshindi wa pili- Dola za Marekani 10,000
-
Nusu fainali- Dola za Marekani 5,000
-
Robo fainali-Dola za Marekani 2,500