Connect with us

 

Timu ya taifa ya soka ya Algeria imeondolewa katika michuano ya kusaka taji la bara Afrika AFCON, kwa kutopata ushindi wowote.

Algeria ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Senegal katika mchuano wake wa kundi B mjini Franceville nchini Gabon siku ya Jumatatu usiku.

Mchuano wa kwanza, Algeria ilitoka sare ya mabao 2-2 na Zimbabwe lakini ikafungwa na Tunisia mabao 2-1.

Mbali na Algeria, Zimbabwe pia imeyaanga mashindano haya baada ya kumaliza wa mwisho katika kundi hilo kwa alama 1.

Mchuano wake wa mwisho, Brave Warriors walishindwa vibaya, baada ya kufungwa na Tunisia mabao 4-2.

Tunisia ilipata mabao yake yote katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo katika dakika ya 9,22,36 na 45 huku Zimbabwe ikijipatia mabao yake katika dakika ya 42 na 58.

Kikosi

Zimbabwe: Mukuruva, Nhamoinesu, Phiri, Zvirekwi, Muroiwa, Bhasera, Mushekwi, Katsande, Musona, Nakamba, Billiat

Tunisia: Jeridi, Ben Youssef, Abdennour, Msakni, Khazri, Khenissi, Maaloul, Sassi, Ben Amor, Naguez, Naim

Siku ya Jumanne, mechi za kutamatisha kundi C zitachezwa katika uwanja wa Oyem.

Morocco itamenyana na Ivory Coast huku Togo ikimenyana na DR Congo, mech zitazochezwa kuanzia saa nne kamili saa za Afrika Mashariki.

Mabingwa watetezi Ivory Coast wanahitaji ushindi katika mchuano wa leo ili kujipa matumaini ya kusonga mbele kwa sababu ina alama 2, huku wapinzani wao wa leo wakiwa na alama tatu.

DR Congo ina alama nne, huku Togo ikiwa ya mwisho kwa alama moja.

Ratiba ya robo fainali

Januari 28 2017

Burkina Faso vs Tunisia-Mechi itacheza katika uwanja wa Libreville

Senegal vs Cameroon-Mechi itachezwa katika uwanja wa Franceville.

Januari 29 2017

Mshindi wa kundi C vs Mshindi wa pili wa kundi D

Mshindi wa kundi D vs Mshindi wa pili wa kundi C

More in