-
-
by
Victor Abuso
Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilipata pigo baada ya kufungwa mabao 2 kwa 0 na Jamhuri ya Afrika ya Kati mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mechi hiyo ilipigwa jijini Bangui na matokeo hayo yamewashangaza wapenzi wa soka nchini DRC. Mabao yote ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yalifungwa katika kipindi cha kwanza, huku bao la kwanza likitiwa kimyani katika dakika 27 kupitia mkwaju wa Penalti uliotiwa kimyani na Vivien Madibe huku Junior Gourrier akifunga bao la pili na la ushindi. Leopard sasa ni ya tatu katika kundi lao kwa alama 3 sawa na Jamhuri ya Kati ambao ni wa pili na kundi hilo linaongozwa na Angola ambayo ina alama nne baada ya kutoka sare ya kutofungana na na Madagascar.
Matokeo kamili ya mwishoni mwa juma: Ijumaa tarehe 4/9/2015 Djibouti 0 Togo 2 Jumamosi 5/9/2015 Comoros 0 Uganda 1 Ushelisheli1 Ethiopia 1 Burundi 2 Niger 0 Namibia 0 Senegal 2 Rwanda 0 Ghana 1 Tanzania 0 Nigeria 0 Boswatana 1 Burkina Faso 0 Sao Tome 0 Morocco 3 Guinea Bissau 2 Congo Liberia 1 Tunisia 0 Sudan Kusini 1 Equatorial Guinea 0 Mauritani 3 Afrika Kusini 1 Gabon 4 Sudan 0 Jumapili tarehe 6 /9/2015 Mauritius 1 Msumbiji 0 Madagascar 0 Angola 0 Swaziland 2 Malawi 2 Zimbabwe 1 Guinea 1 Lesotho 1 Algeria 3 Kenya 1 Zambia 2 Jamhuri ya Afrika ya Kati 2 DRC 0 Chad 1 Misri 5 Sierra Leone 0 Cote d'ivoire 0 Benin 1 Mali 1 Gambia 0 Cameroon 1 Libya 1 Cape Verde 2
Related Topics



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...