Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars iliandikisha matokeo mabaya katika mchuano wake wa ugenini jijini Bissau dhidi ya Guinea Bissau katika mechi muhimu ya kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika nchini Gabon mwaka 2017.
Wenyeji Guinea Bissau, walipata ushindi wa bao 1 kwa 0 Jumatano usiku, bao walilopata dakika ya 18 kipindi cha kwanza kupitia shambulizi la kichwa lilitiwa kimyani na Idrissa Camara.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Estadio 24 de Setembro na ulikuwa mchuano wa kwanza wa kocha Stars Stanley Okumbi.
Mchuano mwingine wa kundi hili kati ya Zambia na Congo Brazaville ulimalizika sare ya bao 1 kwa 1.
Kenya itarudiana na Guinea Bissau siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa ya Nyayo jijini Nairobi.
Congo inaongoza kundi la E kwa alama 5, ikifuatwa na Zambia ambao pia ina lama 5.
Guinea Bissau ni ya tatu kwa alama 4, huku Kenya ikiwa ya mwisho ikiwa na alama 1.
Taifa Stars ya Tanzania, ikiwa ugenini jijini N’Djamena ilipata ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Chad.
Bao la ushindi la Tanzania lilitiwa kimyani na mshambuliaji Mbwana Samatta katika dakika 30 ya kipindi cha kwanza, katika uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya .
Ushindi wa Tanzania unawapa matumaini ya kufuzu katika michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980 wakati fainali hizo zilizofanyika nchini Nigeria.
Mchuano wa marudio ni siku ya Jumatatu wiki ijayo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchuano mwingine wa kundi hili ni kati ya Nigeria na Misri siku ya Ijumaa katika uwanja wa Ahmadu Bello katika jimbo la Kaduna.
Tanzania katika kundi hili wanashikilia nafasi ya 4 baada ya michuano mitatu.
Matokeo mengine ya siku ya Jumatano, Sudan Kusini ikicheza nyumbani jijini Juba mbele ya rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino, ilipoteza mchuano wake dhidi ya Benin baada ya kufungwa mabao 2 kwa 1.
Siku ya Alhamisi.
Madagascar vs Central Africa Republican
Comoros vs Bostwana
Djibouti vs Liberia
Ghana vs Mozambique
Siku ya Ijumaa
Swaziland vs Zimbabwe
Gabon vs Sierra Leon
Nigeria vs Egypt
Mauritania vs Gambia
Cote d’ivoire vs Sudan
Guinea vs Malawi
Tunisia vs Togo
Mali vs Equatorial Guinea
Algeria vs Ethiopia