Fujo za mashabiki katika uwanja wa soka wa Nyayo jijini Nairobi nchini Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita kati ya wenyeji Harambee Stars na Guinea Bissau zilisababisba mchuano wa kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao, kusimamishwa kwa muda wa dakika 30.
Hali hiyo ilianza kushuhudiwa katika dakika 83 baada ya Guinea Bissau kupata bao ambalo wachezaji na mashabiki wa Kenya walidai kuwa mpira haukuwa umevuka mstari baada ya kuguswa na kipa Arnold Origi.
Kenya ambayo pia ilifungwa na Guinea Bisssau bao 1 kwa 0 ugenini mjini Bissau, imejiweka pabaya kuendelea na kampeni ya kufuzu katika michuano hii itakayofanyika nchini Gabon na huenda Shirikisho la soka barani Afrika likaichukua hatua.
Kundi hili linaongozwa na Guinea-Bissau ambayo ina alama 7, mbele ya Congo Brazaville ambayo ina alama 6 sawa na Zambia huku Kenya ikiwa na alama 1. Zambia na Congo Brazaville zilitoka sare ya bao 1 kwa 1.
Matokeo mengine ya Jumapili iliyopita, Ghana ilishindwa kupata ushindi baada ya kutoka sare ya ya kutofugana na Msumbiji jijini Maputo.
Black Stars inaongoza kundi H kwa alama 10, Mauritius ni ya pili kwa alama 6 na ikiwa itashinda siku ya Jumanne dhidi ya Rwanda jijini Kigali bali itaikaribisha Ghana.
Matokeo mengine, Benin wakicheza nyumbani waliwafunga Sudan Kusini mabao 4 kwa 1 huku Bostwana ikiwalemea Comoros kwa mabao 2 kwa 1 .
Katika hatua nyingine, kutokana na timu ya Chad kujitoa katika michuano hii, Shirikisho la soka barani Afrika CAF limepigwa faina ya Dola elfu 20,000 na kufungiwa kutokushiriki michuano ya AFCON kwa mwaka mmoja.
Chad ambayo ilikuwa katika kundi moja la G na Misri, Nigeria na Tanzania ilijiondoa katika dakika za lala salama wakati ikitarajiwa kufika Dar es salaam kwa mchunao wa marudiano siku ya Jumatatu, kwa madai kuwa haikuwa na fedha za kuendelea kushiriki katika michuano hiyo.
Hii inaamana kuwa matokeo yote ya mchuano dhidi ya Chad yamefutwa na sasa zinasalia timu tatu. Misri inaendelea kuwa kileleni kwa alama 4 ikifuatwa na Nigeria ambayo ina alama 2 huku Tanzania ikiwa ya mwisho kwa alama 1.
Mchezo ujao wa Tanzania utakuwa ni mwezi Juni jijini Dar es salaam dhidi ya Misri.
Michuano ya Jumatatu Machi 28 2016
Zimbabwe vs Swaziland
Central Africa Republican vs Madagascar
Libya vs Sao Tome e Principe
Equitoirial Guinea vs Mali
Sierra Leone vs Gabon
Michuano ya Jumanne Machi 29 2016