Connect with us

AFCON 2017: Mambo muhimu katika michuano hii

AFCON 2017: Mambo muhimu katika michuano hii

Mataifa 52 ya Afrika kwa mara nyingine, yanashiriki katika michuano muhimu ya soka kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa itakayofanyika mwaka ujao wa 2017 nchini Gabon.

Mataifa 16, wakiwemo wenyeji Gabon ambao tayari wamefuzu kwa sababu ni wenyeji watashiriki katika michuano hiyo.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano haya, nchi itakayokuwa wenyeji pia inashiriki katika michuano ya kufuzu lakini michuano hiyo itahesabiwa kama ya kirafiki.

Wenyeji Gabon wamejumuishwa pamoja na Sudan, Ivory Coast na Sierre Leone.

Michuano iliyopita, Gabon ilitoka sare ya kutofungana na Ivory Coast mwezi Juni mwaka 2015 na baadaye ikawashinda Sudan mabao 4 kwa 0 mwezi Septemba pia mwaka uliopita.

Wiki hii, Gabon umeratibiwa kucheza na Sierra Leon.

Mshindi wa kundi hili ndiye atakayefuzu katika fainali ya AFCON kwa sababu ina timu tatu ambazo alama zake zinahesabiwa.

Mbali na hili, kuna makundi 13 na mshindi katika kila kundi atafuzu lakini timu 2 zitakazokuwa zimemaliza katika nafasi ya pili kwa matokeo mazuri pia yatafuzu na kuungana pia na Gabon.

Hadi sasa mabao 126 yamefungwa tangu kuanza kuchezwa kwa michuano hii ya kufuzu mwezi Juni mwaka uliopita.

Wachezaji wanaoongoza katika safu ya ufungaji ni pamoja na El Arbi Hillel Soudani kutoka Algeria, Ferebory Dore kutoka Congo Brazavile na Basem Morsy ya Misri kila mmoja amefunga mabao manne.

Eritrea na Somalia ndizo mataifa pekee ambayo hayashiriki katika michuano hii.

More in